Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yaamua kuachana na Marc Guehi

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Wiki iliyopita ilishindwa kukamilisha dili la Pauni milioni 35 kwa ajili ya mchezaji huyo na sasa wanapanga kumsubiri hadi mkataba wake utakapokoma mwakani.

MABOSI wa Liverpool wamefikia makubaliano  hawatowasilisha ofa yoyote ili kumsajili beki wa kati wa Crystal Palace, Marc Guehi, 25, dirisha dogo la usajili la Januari na badala yake watasubiri hadi mwisho wa msimu ili kumpata akiwa huru.

Wiki iliyopita ilishindwa kukamilisha dili la Pauni milioni 35 kwa ajili ya mchezaji huyo na sasa wanapanga kumsubiri hadi mkataba wake utakapokoma mwakani.

Ripoti zinaeleza tetesi zinazosambaa kwa sasa kuna klabu nyingine zinazotaka kumsajili Guehi ifikapo Januari, Liverpool inaona ni mbinu ya Palace ili kuirejesha mezani na hataki aondoke bure mwisho wa msimu, hivyo inataka kulazimisha kumuuza Januari.

Kwa mujibu wa takwimu, Guehi amekuwa mmoja wa mabeki wenye kiwango bora EPL msimu huu akiwa na wastani wa usahihi wa pasi kwa asilimia 89. Msimu huu amecheza mechi sita za michuano yote.


Ibrahima Konate

LIVERPOOL ipo katika mazungumzo na wawakilishi wa beki wao wa kimataifa wa Ufaransa, Ibrahima Konate, 26, kwa ajili ya kumsainisha mkataba mpya dirisha hili. Konate ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu anahusishwa sana na Real Madrid ambayo inataka kumsajili kama mchezaji huru. Beki huyu yupo tayari kusaini mkataba mpya lakini anahitaji ongezeko maradufu la mshahara.


Mohamed Salah

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Kylian Mbappe, 26, ameripotiwa kumshawishi staa wa Liverpool, Mohamed Salah, 33, kujiunga naye dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Salah alisaini mkataba mpya wa miaka miwili na Liverpool Aprili mwaka huu, lakini ahadi ya kucheza Bernabeu inaweza kumshawishi akaomba kuondoka. Liverpool tayari imeshaanza kujipanga na maisha bila staa huyo na iliwasajili Alexander Isak na na Hugo Ekitike.


Andre Onana

KIPA wa Manchester United, Andre Onana, 29, atapokea mshahara mara mbili zaidi ya ule anaoupokea kwa sasa baada ya kufikia makubaliano ya kujiunga na Trabzonspor ya Uturuki kwa mkopo. Onana ambaye atasafiri kwenda Uturuki, Alhamisi ya wiki hii kwa sasa anakunja Pauni 120,000 kwa wiki na akitua Trabzonspor atakuwa akipata Pauni 240,000 kwa wiki.


Jean-Philippe Mateta

ASTON Villa, Leeds United na Newcastle United zinafuatilia kwa karibu huduma ya mshambuliaji wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta, 28, dirisha lijalo. Mateta alikuwa akitajwa sana kuhitajika na Manchester United dirisha lililopita kabla ya vigogo hao kuachana na mpango wa kutaka kumsajili. Mateta ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Palace.


Dele Alli

KIUNGO Dele Alli, 29, ambaye yupo sokoni kama mchezaji huru baada ya kuachana na klabu ya Como ya Italia, anawindwa na  Birmingham City, Wrexham na West Bromwich Albion zinazoshindana kumchukua bure.  Licha ya kuporomoka kiwango, timu hizo zinaamini Alli anaweza kuwasaidia katika harakati zao za Ligi Daraja la kwanza England msimu huu.


Christos Mandas

KIPA wa Lazio, Christos Mandas, 23, anatafikiria kuondoka dirisha hili baada ya kupoteza namba kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Wolves inafikiria kumsajili staa huyu dirisha lijalo la majira ya baridi baada ya kujaribu kumchukua dirisha lililopita la majira ya kiangazi na kushindikana. Mabosi wa Wolves waliwasilisha ofa ya Pauni 17.3 milioni ambayo ilikataliwa.


Denzel Dumfries

BEKI kisiki wa Inter Milan na timu ya taifa ya Uholanzi, Denzel Dumfries, 29, ambaye dirisha lililopita alikuwa akihusishwa na Manchester United, ameweka wazi anatamani sana kucheza Ligi Kuu England kwani ni ndoto yake. Dumfries ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028,msimu uliopita alicheza mechi nne za michuano yote.