Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool imeshika Pauni 120 milioni kumnasa Isak

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Kinachoelezwa ni miamba hiyo ya Anfield imetenga kiasi cha kutosha kwenye mpango wao wa kumsajili straika wa Newcastle United na Sweden, Alexander Isak huku ikiamini itahitaji kuwa na Pauni 120 milioni au zaidi kumpata mchezaji huyo.

LIVERPOOL imeripotiwa kuwa na ufahamu straika anayemsaka kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi atawagharimu mkwanja usiopungua Pauni 120 milioni.

Kinachoelezwa ni miamba hiyo ya Anfield imetenga kiasi cha kutosha kwenye mpango wao wa kumsajili straika wa Newcastle United na Sweden, Alexander Isak huku ikiamini itahitaji kuwa na Pauni 120 milioni au zaidi kumpata mchezaji huyo.

Hata hivyo, ukiweka kando ishu hiyo ya pesa, Liverpool italazimika pia kushinda upinzani kutoka kwa vigogo wenzake wa Ligi Kuu England, Chelsea na Arsenal ambazo pia zimeweka wazi kuhitaji saini ya mshambuliaji huyo anayecheza kwa kiwango kikubwa msimu huu.

Utamu unazidi kunoga kutokana na ukweli Chelsea na Arsenal zote ni timu zisizoogopa kufungua pochi kusajili mchezaji mpya kitu ambacho kitawafanya Liverpool kufanya haraka kumalizana na staa huyo wa St James’ Park mapema.



Lamine Camara

TOTTENAHM Hotspur imeripotiwa italazimika kupambana mbele ya Liverpool, Manchester City na Chelsea katika mchakamchaka wa kuwania huduma ya kiungo wa AS Monaco, Lamine Camara kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya. Staa huyo wa Senegal mwenye umri wa miaka 21 ni mmoja wa wachezaji wenye viwango vikubwa msimu huu na ndiyo maana timu kibao zinahitaji huduma yake.



Benjamin Sesko

CHELSEA imeripotiwa kuingia vitani katika mchakamchaka wa kumsajili straika wa RB Leipzig na Slovenia, Benjamin Sesko katika dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 21, amekuwa pia kwenye rada za timu ya Arsenal, ambayo kocha wake Mikel Arteta amekuwa akihaha kutafuta saini ya mshambuliaji mpya kwenye dirisha lijalo na fowadi huyo wa Bundesliga yupo kwenye mpango.


Castello Lukeba

CHELSEA na Liverpool zimeripotiwa zitaingia kwenye vita kali ya kumsaka beki wa kati wa RB Leipzig, Castello Lukeba, ambaye amekuwa kwenye kiwango kikubwa sana msimu huu. Miamba hiyo ya Ligi Kuu England itakwenda jino kwa jino kwenye msako wa mchezaji huyo wakati wa dirisha lijalo la uhamisho wa dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. Real Madrid pia inamtaka beki huyo mwenye miaka 22.


Florian Wirtz

BOSI wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amefichua kwamba vinara hao wa Bundesliga wanampango wa kumsajili mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz, 21. Kinachoripotiwa ni fowadi huyo Mjerumani amekuwa akiwindwa pia na miamba ya soka ya Ligi Kuu England, Manchester City jambo litanalofanya kuwapo na uwezekano mkubwa wa kushindania saini yake wakati dirisha litakapofunguliwa.


Antony

REAL Betis inafikia mchakato wa kumchukua jumla winga wa Kibrazili, Antony, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo akitokea Manchester United. Betis imevutiwa na maendeleo ya mchezaji huyo kwenye timu yao, hivyo wanapiga hesabu za kumchukua jumla mwishoni mwa msimu huu wakati dirisha la usajili la majira ya kiangazi litakapofunguliwa. Antony anaweza kuuzwa kwa Pauni 41 milioni.


Alejandro Garnacho

BARCELONA inaripotiwa kumfuatilia kwa karibu winga wa Manchester United, Alejandro Garnacho, 20, ili kunasa saini yake dirisha lijalo. Barcelona inamtazama Garnacho kama mchezaji anayeweza kwenda kufanya vizuri kwenye kikosi chao huku ikitambua wazi tatizo la kifedha linaloigharimu Man United kwa sasa watakubali kuumuza Muargentina huyo.


Carlos Baleba

LIVERPOOL inaripotiwa kumfukuzia kiungo mkabaji wa Brighton,  Carlos Baleba ikihitaji huduma yake dirisha lijalo la usajili. Liverpool inaamini staa huyo,21, kutoka Cameroon anafiti kwenye staili yao ya uchezaji hivyo wanahitaji akakipige Anfield kuanzia msimu ujao wa 2025/26 ili kuendeleza ubora wao wa msimu huu wa 2024/25.