Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kylian Mbappe aingia anga za kibabe

MBAPPE Pict

Muktasari:

  • Staa huyo wa Real Madrid alifunga bao la kwanza kwenye ushindi wa 2-1 iliyopata timu hiyo uwanjani Bernabeu dhidi ya mahasimu wao Barcelona, jana Jumapili, Oktoba 26.

MADRID, ENGLAND: SUPASTAA, Kylian Mbappe ameingiza jina lake kwenye orodha ya mastaa matata kabisa waliowahi kucheza kwa viwango vya kibabe kwenye mechi za El Clasico.

Staa huyo wa Real Madrid alifunga bao la kwanza kwenye ushindi wa 2-1 iliyopata timu hiyo uwanjani Bernabeu dhidi ya mahasimu wao Barcelona, jana Jumapili, Oktoba 26.

Mbappe alifunga bao hilo baada ya pasi nzuri kutoka kwa Jude Bellingham. Kwa bao hilo, limemfanya Mbappe kuwa mchezaji wa tatu kufunga kwenye mechi nne mfululizo za El Clasico.

Mastaa wengine wawili waliowahi kufanya hivyo ni wakali Cristiano Ronaldo na Ronaldinho.

LAMI 01

Ronaldinho alifunga mara nne mfululizo kwenye mechi kati ya 2004 na 2006, wakati mshindi mara tano wa Ballon d’Or, Ronaldo alifunga bao lake la saba katika mechi dhidi alicheza dhidi ya Barcelona alipokutana nao 2012.

Baada ya bao la Mbappe, Barca ilisawazisha kupitia kwa Fermin Lopez baada ya krosi ya chinichini ya Marcus Rashford, Madrid iliongeza jingine lililofungwa na Bellingham.

Katika umri wa miaka 22 na siku 119, Bellingham, anakuwa mchezaji mwenye umri mdogo wa Madrid kufunga na kuasisti katika mechi ya El Clasico katika karne ya 21.

LAMI 02

Katika mchezo huo, Vinicius Jr alionyeshwa kutoridhishwa baada ya kutolewa na kocha Xabi Alonso, lakini kasi yake ya uwanjani ilimfanya kiungo Pedri amvute jezi na kuonyeshwa kadi ya njano kabla ya kuonyeshwa njano nyingine na kuwa nyekundu alipomfanyia rafu Aurelien Tchouameni kwenye dakika za majeruhi za mchezo huo.

Ushindi huo unaifanya Madrid kujitanua kwenye kilele cha msimamo wa LaLiga ikiweka pengo la pointi kufikia tano dhidi ya mahasimu wao hao wa Nou Camp.

Wakati huo, Mbappe akiwa kwenye wakati wake mzuri baada ya kufunga bao lake la 12 msimu huu katika mechi tisa alizokabiliana na Barcelona. Na sasa amejiweka kwenye wakati mzuri wa kuwa mchezaji aliyefunga mara nyingi dhidi ya Barca katika karne ya 21, rekodi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Ronaldo, ambaye amefunga zaidi ya mabao 20 dhidi ya Barca katika mechi 34.

Gwiji mwingine wa Madrid, Karim Benzema amefunga mabao 16 katika mechi 46 dhidi ya Barca.