Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

El Clasico ya kivingine itapigwa Estadio Santiago Bernabeu

EL CLASICO Pict

Muktasari:

  • Safari hii, mechi hiyo ya El Clasico itafanyika Estadio Santiago Bernabeu, Jumapili. Je, kuna kipya kitatokea? Mabingwa watetezi wa LaLiga, Barca watakwenda kuwakabili mahasimu wao hao wakiwa nyuma kwa pointi mbili kileleni kwenye msimamo wa ligi.

MADRID, HISPANIA: HAKUNA kitu kinachobamba mashabiki kama El Clasico. Mara zote kinapopigwa kipute cha Real Madrid na Barcelona, macho na masikio ya mashabiki wa soka duniani kote, vyote vinaelezwa mahali panapofanyika shughuli hiyo pevu.

Safari hii, mechi hiyo ya El Clasico itafanyika Estadio Santiago Bernabeu, Jumapili. Je, kuna kipya kitatokea? Mabingwa watetezi wa LaLiga, Barca watakwenda kuwakabili mahasimu wao hao wakiwa nyuma kwa pointi mbili kileleni kwenye msimamo wa ligi.

Kocha wa Real Madrid, Xabi Alonso, kiungo gwiji wa klabu hiyo ambaye alishinda La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya alipokuwa mchezaji wa Los Blancos kwa miaka mitano, atakumbana na joto la kuikabili Barcelona kwa mara ya kwanza kwenye El Clasico.

Na anaamini atatoka kimasomaso kutokana na kuwa na huduma ya straika Kylian Mbappe, ambaye yupo kwenye kiwango bora kabisa kwa sasa.

Kocha wa Barcelona, Hansi Flick, kwa upande wake, msimu uliopita aliinyanyasa sana Real Madrid na alishinda mechi zote nne katika msimu wake wa kwanza katika timu hiyo.

Kinda Lamine Yamal alikuwa miongoni mwa mastaa waliofanikisha ushindi wa mechi zote hizo na huenda akaendelea kuwa mwiba mchungu tena kwa Los Blancos.

EL 03

Mambo yapoje kwenye ‘head-to-head’

Real Madrid imekuwa na faida ya kushinda mara nyingi dhidi ya Barcelona kwenye rekodi zao walizokutana tangu miaka 1930. Rangu wakati huo, klabu hizo zimegawanya miaka ya kutawala soka na Madrid ilikuwa miaka ya 1960, na Barca miaka ya 1970 na 1980.

Lakini, mambo yalianza kwenda sawa miaka 20 iliyopita na rekodi za Madrid kwenye mechi walizokutana na Barcelona, zilipungua katika kipindi cha Kocha Pep Guardiola alipokuwa Camp Nou. Madrid ilishinda mara moja tu katika mechi 14 za michuano yote ilipokutana na Barca kati ya 2008 na 2012, hapo ikiwamo ushindi wa 6-2 na 5-0 iliyopata Barca ya Guardiola, sambamba na ule ushindi wa kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Tangu wakati huo, Barca ilionekana kuimudu zaidi Madrid na haijapoteza kwenye mechi saba za El Clasico kuanzia 2017 hadi 2019, kabla ya Madrid yenyewe kutopoteza kwenye mechi sita kati ya 2019 na 2022.

Lakini, ushindi mara nne wa Barca msimu uliopita, umewafanya kupunguza pengo kwa kiasi kikubwa kwenye rekodi za head-to-head.

Sasa Madrid imeshinda 105 na Barcelona imeshinda 104, tofauti mechi moja tu, huku timu hizo zikitoka sare kwenye mechi 52.

EL 02

Nini kilitokea msimu uliopita?

Barca, isivyotarajiwa, ilijipigia Madrid kama inavyotaka msimu uliopita. Barca ilianza msimu na maswali mengi na wengi walikuwa hawafahamu kocha Flick atafanya nini na kikosi hicho kilichokuwa na vijana wengi.

Wakati huo, wenzao Madrid, walikuwa wametokea kushinda taji la LaLiga na Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku wakimwongeza Mbappe kwenye kikosi chao.

Lakini, ilipofika mechi ya El Clasico hali ilikuwa tofauti.

Barca ilikuwa bora sana kwenye safu yake ya ushambuliaji, ikifunga mabao 16 katika mechi nne ilizokabiliana na Madrid, ikishinda kwenye mechi zote mbili za ligi, fainali ya Copa del Rey na kwenye Spanish Supercopa.

Katika mechi hizo, Barca ilionekana kama inaweza kutikisa nyavu za Madrid kwa kadri inavyotaka.

Kuna mechi moja, Mbappe aliitanguliza Madrid 2-0 ndani ya dakika 15, Barca ilijibu mapigo kwa kufunga mara nne kabla ya mapumziko. Ilifunga mara nne pia kipindi cha pili uwanjani Bernabeu, Oktoba mwaka jana na mara nne kwenye kipindi cha kwanza katika ushindi wa 5-2 katika Supercopa, Januari mwaka huu.

Kwa jumla, Barca imefunga mabao 16-7 dhidi ya Madrid kwenye El Clasico.

EL 01

Bato zinazosubiriwa

Vita ya kwanza kwenye El Clasico ya Jumapili itakuwa kati ya Mbappe na washambuliaji wa Barca.

Vita hii itakuwa juu ya nani atafunga mara nyingi. Msimu uliopita, mechi iliyofanyika Bernabeu ilimalizika kwa Barca kushinda 4-0, huku mabao yote yakifungwa kipindi cha pili. Lakini, kwenye kipindi cha kwanza, mambo yalikuwa tofauti, Mbappe alikuwa msumbufu sana kwa Barca na aliotea mara sita.

Baada ya hapo, Mbappe alionekana kama kutegua mtego wa mabeki wa Barcelona na nusura awafanye vibaya kwenye mchezo uliofuatia, alipofunga mara mbili, lakini shukrani kwa washambuliaji wa Barcelona waliokoa jahazi.

Vita nyingine inayotazamiwa kutokea ni ile ya Lamine Yamal na Alvaro Carreras. Hilo ni eneo jingine linalotazamiwa kuwa na upinzani mkali katika dakika 90 za mchezo huo na Barca itahitaji huduma ya mkali wao, Yamal kuwa ya kiwango cha juu kutokana na kuwakosa wachezaji wao muhimu waliowasaidia msimu uliopita, Raphinha, Robert Lewandowski na Dani Olmo.

Mechi hiyo itakuwa mtihani muhimu kwa Marcus Rashford kuonyesha ubora wake katika mechi kubwa ya upinzani mkali baada ya kufanya hivyo mara kadhaa kwenye Manchester derby, alipochuana na Manchester City akiwa Manchester United.