Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa hizi rekodi NBA tema mate chini

Muktasari:

  • Kutoka enzi za Bill Russell na Wilt Chamberlain hadi zama za Michael Jordan na Kobe Bryant, na sasa kizazi cha LeBron James na Stephen Curry kila nyota ameandika historia. Hata hivyo, kuna rekodi chache ambazo zinavuka upeo wa kawaida na kuwa ngumu kuvunjwa na hizi ni miongoni.

WASHINGTON, MAREKANI: KILA msimu mpya wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) huibua mjadala kuhusu nani ataibuka na kuwa gumzo, timu ipi itatawala na rekodi zipi zitavunjwa.

Lakini, katika historia ya ligi hiyo kongwe ya kikapu duniani kuna baadhi ya rekodi ambazo zimekuwa ngumu kuvunjwa zikisalia kuwa alama ya kumbukumbu za mchezo huo.  Tangu kuanzishwa 1946, NBA imezalisha magwiji walioacha alama kwenye mchezo.

Kutoka enzi za Bill Russell na Wilt Chamberlain hadi zama za Michael Jordan na Kobe Bryant, na sasa kizazi cha LeBron James na Stephen Curry kila nyota ameandika historia. Hata hivyo, kuna rekodi chache ambazo zinavuka upeo wa kawaida na kuwa ngumu kuvunjwa na hizi ni miongoni.


CHAMBERLAIN (POINTI 100) 

Fikiria mchezo wa kikapu ambapo wachezaji hufunga pointi 20 au 30 na kuonekana mashujaa. Lakini, jiweke kwenye kiti Machi 2, 1962 huko Hershey, Pennsylvania ndipo alipotokea Wilt Chamberlain, mchezaji mwenye kimo cha futi 7 na inchi 1 akafanya kitu ambacho hadi leo hakijarudiwa kufunga pointi 100 kwenye mechi moja. Hakukuwa na televisheni wala kamera za kisasa. Habari zilienea kupitia magazeti. Taarifa ya mwisho ilikuwa ‘Philadelphia Warriors 169 New York Knicks 147’, lakini kinachoendelea kukumbukwa ni takwimu za mwamba huyo. Kwa nini ni ngumu kuvunjwa? Mchezo wa sasa makocha wamekuwa wakihimiza pasi na nidhamu kuliko mchezaji mmoja kushambulia kila dakika.

Jambo lingine ni ratiba na afya ya wachezaji. Mchezaji anaweza kufunga pointi 50 au 60, lakini kufika 100 inahitaji dakika nyingi uwanjani. Unajua hiyo ni nini? Ni utaratibu wa kupunguza idadi ya mechi au dakika ambazo mchezaji anacheza ili kulinda mwili na kuzuia majeraha. Jambo lingine ni teknolojia na mbinu zimefanya ugumu kwa mchezaji mmoja kutawala kiwango kikubwa mchezo. Kobe Bryant alijaribu 2006 dhidi ya Toronto Raptors na kufunga pointi 81, lakini ilikuwa ngumu kufikia 100. Wachezaji kama Luka Doncic au Devin Booker wana uwezo mkubwa wa kufunga, lakini rekodi ya Chamberlain inabaki kuwa kama mlima Kilimanjaro unaweza kuutazama, lakini kuupanda ni shughuli nzito.


MATAJI YA CELTIC (1959–1966)

Kwenye NBA Boston Celtics chini ya Bill Russell kuanzia 1959 hadi 1966 ilinyakua mataji manane mfululizo ya NBA.

Hizo zilikuwa enzi ambazo Celtics ilikuwa bora. Ilicheza kwa nidhamu ikiongozwa na Russell ambaye alikuwa si tu mlinzi bora, bali pia kiongozi kwa wachezaji wenzake. Kwa nini ni ngumu kuvunjwa? Leo kuna timu nyingi zenye nyota mahiri - Denver Nuggets, Milwaukee Bucks, Golden State Warriors jambo linalofanya iwe vigumu timu moja kutawala muda mrefu. Hoja nyingine wachezaji wanabadili timu mara kwa mara wakitafuta malipo au nafasi bora ya ubingwa. Hii inaathiri ubora wa timu moja kubaki pamoja muda mrefu. Kwa miaka ya karibuni hata timu bora zaidi hupata ubingwa mara mbili au tatu mfululizo, lakini kufika nane? Hiyo ni ndoto.


A.C GREEN (1986–2001)

Kuanzia 1986 hadi 2001, Amanda Chester Green maarufu A.C Green alicheza mechi 1,192 mfululizo bila kukosa hata moja. Hii ni rekodi ya ajabu ukizingatia ushindani uliopo NBA ukiambata na safari ndefu za ndege, ratiba ngumu za mechi 82 kwa msimu, majeraha na maradhi. Green hakuwa mfungaji wa pointi nyingi wala staa wa kuripotiwa mara kwa mara, lakini alijulikana kwa utimamu. Alikuwa mchezaji anayejitolea kwa ajili ya timu bila kujali changamoto. Kwa nini ni ngumu kuvunjwa rekodi yake? Changamoto kubwa ni ishu ya mazingira. Unajua kwanini? Katika miaka ya sasa makocha na madaktari wanapanga wachezaji kukosa baadhi ya mechi makusudi ili kulinda afya zao. Ishu nyingine ni majeraha ya mara kwa mara. Kasi na nguvu ya ligi hiyo kwa kisasa inasababisha wachezaji wengi kupata majeraha ya misuli, magoti au mgongo.