Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa Amorim chochote kinatokea

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Kinachoripotiwa ni kwamba huko Old Trafford mabosi wa timu hiyo wamefanya mazungumzo na baadhi ya mastaa wakubwa kwenye kikosi cha Man United kujadili hali ya mambo ilivyo katika timu hiyo.

MANCHESTER, ENGLAND: MAMBO ni moto. Ligi Kuu mbalimbali zimesimama kupisha mechi za kimataifa, lakini kipindi hiki kimekuwa cha presha kubwa kwa kocha Ruben Amorim juu ya usalama wa kibarua chake huko Manchester United.

Kinachoripotiwa ni kwamba huko Old Trafford mabosi wa timu hiyo wamefanya mazungumzo na baadhi ya mastaa wakubwa kwenye kikosi cha Man United kujadili hali ya mambo ilivyo katika timu hiyo.

Amorim, 40, anakaribia kufikisha mwaka wake wa kwanza tangu alipotua Old Trafford, akiwa amerithi mikoba ya kuinoa miamba hiyo kutoka kwa Mdachi Erik ten Hag, Novemba 2024.

AMO 01

Hata hivyo, baada ya kuiongoza Man United kushika nafasi ya chini zaidi kuwahi kutokea kwenye Ligi Kuu England, namba 15 msimu uliopita  timu imekuwa na maendeleo ya kusuasua tofauti na ilivyotarajiwa.

Msimu huu pia Man United imeanza kwa kasi hafifu, ikitupwa nje kwenye Kombe la Ligi tena na timu ya League Two, Grimsby Town. Wakati kikosi hicho cha Amorim kikiwa bado hakijapata ushindi wowote ugenini kwa msimu huu, mabosi wakubwa wa klabu wameanza kuzungumza na baadhi ya wachezaji kutambua hali ya mambo inavyoendelea kwenye timu hiyo.

MAN 01

Hili linafanana na lile tukio la kikao cha saa saba baina ya Ten Hag na mabosi wake wa zamani kipindi kama hiki mwaka jana. Na baada ya kikao hicho haikuchukua muda mrefu kocha huyo alifunguliwa mlango wa kutokea.

Mmiliki mwenza, Joel Glazer, ofisa mkurugenzi mtendaji Omar Berrada, mkurugenzi wa michezo, Dan Ashworth mkurugenzi wa ufundi, Jason Wilcox wote walikutana kwenye ofisi za bilionea Sir Jim Ratcliffe za Knightsbridge huko London kujadili mwenendo wa timu.

Mjumbe wa bodi, Jean-Claude Blanc, ofisa mwendeshaji mkuu, Collette Roche na ofisa mkuu wa idara ya fedha, Roger Bell nao wanaripotiwa kuwapo kwenye kikosi hicho.

MAN 02

Ten Hag alidumu kwa wiki tatu tu baada ya kikao kizito cha saa saba. Na hii inaweza isichukue muda mrefu pia kabla ya vigogo wa Man United kufanya uamuzi mgumu endapo kama matokeo ya uwanjani ya timu yakishindwa kubadilika.

Kinachoripotiwa ni kwamba mabosi Berrada na Wilcox ndio vinara wa mjadala huo huo ambapo wamekuwa kiunganishi cha mabosi na mambo ya uwanjani. Nahodha wa Man United, Bruno Fernandes ni miongoni mwa wachezaji waliohusishwa kwenye mjadala, huku kuna wengine pia waliripotiwa kuombwa maoni yao juu ya mwenendo wa timu.

Mmiliki mwenza wa Man United, bilionea Ratcliffe mara kadhaa amekuwa akijibu maswali ya kuhusu hatima ya kocha Amorim. Tajiri huyo wa kampuni ya Ineos amekuwa akimtetea kocha huyo, jambo linalothibitisha Amorim bado anaungwa mkono na mabosi wake.

AMO 03

“Hakuwa na misimu mizuri,” amesema Ratcliffe akielekezea hatima ya kocha Amorim.

“Ruben anahitaji kuonyesha ubora wa ukocha wake kwa miaka mitatu.”

Makocha kadhaa wameanza kuhusishwa na kibarua hicho cha kurithi mikoba ya Amorim huko Old Trafford ni pamoja na Oliver Glasner, Eddie Howe, Gareth Southgate na Diego Simeone.

Licha ya kuisimamia Man United kwenye mechi 50 za Ligi Kuu England kocha Amorim bado hajawahi kushinda mechi mfululizo kwenye ligi hiyo. Man United ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sunderland nyumbani uwanjani Ole Trafford, lakini rekodi yao ya ugenini imekuwa ya hovyo na hiyo imekuwa ikitishia.

AMO 02

Man United kwa sasa inashika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, pointi mbili nyuma ya nafasi sita za juu na ratiba ya mechi zao zijazo ni ya moto kwelikweli.

Itaanza kuikabili Liverpool kisha Brighton, Nottingham Forest na Tottenham Hotspur katika mechi kali za EPL zinazofuata mfululizo.