Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuyt aichukua Fenerbahce kabla ya kuivaa Liverpool

KUYT Pict

Muktasari:

  • Kuyt, mwenye umri wa miaka 46, amepandishwa kutoka nafasi ya kocha msaidizi baada ya Ismail Kartal kujiuzulu kufuatia kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Galatasaray, Jumatatu.

INSTABUL, UTURUKI: KOCHA wa muda wa Fenerbahce, Dirk Kuyt, ameteuliwa kushika nafasi hiyo wiki moja kabla ya kukutana na timu yake ya zamani Liverpool katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kuyt, mwenye umri wa miaka 46, amepandishwa kutoka nafasi ya kocha msaidizi baada ya Ismail Kartal kujiuzulu kufuatia kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Galatasaray, Jumatatu.

Katika taarifa yake, Fenerbahce imesema Kuyt ataendelea kuwa kocha wa muda hadi hapo kocha mkuu mpya atakapoteuliwa.

KUY 01

Kuyt si mgeni katika klabu hiyo ya Uturuki, kwani aliwahi kuitumikia kama mchezaji na kusaidia kutwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2013/14.

Mechi yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Goztepe katika Ligi Kuu ya Uturuki Jumamosi, kabla ya Fenerbahce kuikaribisha Liverpool Jumatano, Novemba 4, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kuyt anaifahamu vizuri Liverpool, baada ya kuitumikia klabu hiyo ya Anfield kwa miaka sita. Akiwa na kikosi hicho, alifunga mabao 71 katika mechi 285 na kusaidia kutwaa Kombe la Ligi mwaka 2012.

KUY 02

Baada ya kuondoka Liverpool, alijiunga na Fenerbahce na kuitumikia kwa miaka mitatu, kabla ya kurejea Feyenoord. Alistaafu kucheza soka mwaka 2017.

Baadaye alianza safari ya ukocha, akizifundisha ADO Den Haag, Beerschot na FC Dordrecht, kabla ya kurejea Fenerbahce Juni 2026 akiwa kocha msaidizi.

Kuyt anakabidhiwa jukumu hilo wakati Fenerbahce ikiwa nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ya Uturuki, ikiwa nyuma kwa pointi sita dhidi ya vinara Galatasaray.