Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kundi C WAFCON kuna mechi za kupona au kufa

Muktasari:

  • Nigeria na Misri zitakutana kwenye Uwanja wa Rabat Olympic Stadium kuanzia saa 21:00 usiku, wakati Malawi na Zambia zitapambana muda huohuo kwenye Uwanja wa Al Medina, Rabat.

HATUA ya makundi kwenye kundi C linakwenda kutamatika leo kwa mechi mbili kupigwa Nigeria itaikabili Misri na Malawi ikikipiga dhidi ya Zambia katika mechi zitakazoamua timu zitakazovuka kwenda robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake, WAFCON 2026.

Nigeria na Misri zitakutana kwenye Uwanja wa Rabat Olympic Stadium kuanzia saa 21:00 usiku, wakati Malawi na Zambia zitapambana muda huohuo kwenye Uwanja wa Al Medina, Rabat.

Ratiba hiyo imethibitishwa na Shirikisho la Soka Afrika CAF, huku mechi zote zikichezwa kwa wakati mmoja ili kulinda usawa wa ushindani katika kundi.

Nigeria inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kazi kubwa baada ya kuanza mashindano kwa kushtukizwa na Malawi, ikipokea kichapo cha mabao 3-2. Mabao ya Temwa Chawinga na Tabitha Chawinga yaliipa Malawi ushindi huo mkubwa dhidi ya mabingwa watetezi, kabla Nigeria kurejea kwenye ushindani kwa kuifunga Zambia 1-0 katika mchezo wa pili.

Kwa upande wa Zambia, Copper Queens ilianza mashindano kwa kishindo baada ya kuichapa Misri mabao 6-0, mchezo ambao Barbra Banda alifunga mabao manne na kuonyesha kiwango bora. Hata hivyo, Chama hilo lilipoteza 1-0 dhidi ya Nigeria. Hivyo, mchezo wa Malawi dhidi ya Zambia utakuwa wa aina yake kwa sababu Malawi imeonyesha kuwa si timu ya kupewa nafasi ndogo baada ya kuwashangaza mabingwa watetezi Nigeria.

Kwa Zambia, ushindi unaweza kuipa nafasi nzuri ya kumaliza kileleni mwa kundi, lakini itahitaji kuwa makini dhidi ya timu ambayo tayari imeonyesha uwezo wa kufunga katika hatua muhimu za mchezo.

Nayo Nigeria inajua kuwa mchezo dhidi ya Misri si rahisi licha ya kupoteza mechi mbili za makundi. Super Falcons, ambao ni mabingwa watetezi, wanahitaji matokeo mazuri ili kujihakikishia nafasi ya kwenda robo fainali.

Malawi iko kileleni mwa kundi ikiwa na pointi sita, Nigeria ikiwa nafasi ya pili na pointi tatu sawa na Zambia zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa huku Misri ikisalia mkiani bila pointi.