Konate akataa Liverpool, aisubiria Real Madrid
Muktasari:
- Inaelezwa beki huyu kisiki anataka kujiunga na Real Madrid mwisho wa msimu na anaona kutosaini mkataba mpya itakuwa ni jambo zuri kwake kwani haitomsumbua kukamilisha uhamisho huo.
BEKI kisiki wa Liverpool na timu ya taifa ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 26, Ibrahima Konate, ameamua kutosaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Anfield baada ya mkataba wake kumalizika mwisho wa msimu huu.
Inaelezwa beki huyu kisiki anataka kujiunga na Real Madrid mwisho wa msimu na anaona kutosaini mkataba mpya itakuwa ni jambo zuri kwake kwani haitomsumbua kukamilisha uhamisho huo.
Awali iliripotiwa beki huyu anahitaji kiasi kikibwa cha pesa kama mshahara ili asaini dili jipya lakini sasa mambo yanaonekana kubadilika kwani hataki kabisa kubaki.
Hata hivyo, mabosi wa Liverpool bado hawajakata tamaa na wanaendelea kufanya mazungumzo kwa ajili ya kumshawishi akubali ofa yao.
Mshahara wa sasa wa Konate ni Pauni 80,000 kwa wiki na inaelezwa aliwaambia Liverpool anataka Pauni 200,000 kwa wiki.
Michael Olise
BAYERN Munich inahitaji takribani Pauni 100 milioni kwa ajili ya kiungo wao wa kimataifa wa Ufaransa Michael Olise, mwenye umri wa miaka 23, ambaye hivi karibuni Liverpool imeripotiwa kuhitaji huduma yake. Mabosi wa Bayern wanahitaji kiasi hicho kwa sababu mkataba wa Olise bado mrefu, unamalizika mwaka 2029, pia ni mmoja kati ya wachezaji wao tegemeo. Liverpool inamhitaji ili akazibe pengo la Mohamed Salah anayeweza kuuzwa mwisho wa msimu huu.
Marc Guehi
CHELSEA inatazamia kumsajili beki kisiki wa Crystal Palace, Marc Guehi kutoka Crystal Palace na kipa wa AC Milan, Mike Maignan kwa usajili huru dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Dirisha lililopita, Chelsea ilitamani kumsajili Maigan lakini ofa yao ilikataliwa na Milan kwa sababu lilikuwa ndogo. Guehi ambaye dili lake la kujiunga na Liverpool lilifeli dakika za mwisho za dirisha lililopita, itaanza naye mazun ingawa kuna ushindani kutoka timu nyingine ambazo zinamhitaji.
Bernardo Silva
RIPOTI zinaeleza Manchester City haina mpango wa kumsainisha mkataba mpya kiungo wao mkongwe Bernardo Silva, hivyo anaweza kuondoka bure dirisha lijalo la majira ya kiangazi na Juventus na Benfica zimeonyesha nia ya kumhitaji. Silva anamaliza mkataba wake na Man City mwisho wa msimu huu na siku chache zilizopita mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais Benfica alisema akipita kitu cha kwanza ni kuhakikisha Silva anatua.
Ayyoub Bouaddi
LIVERPOOL, Arsenal na Manchester United ni miongoni mwa klabu zinazoiwania saini ya kiungo wa Lille Ayyoub Bouaddi mwenye umri wa miaka 17. Hadi sasa, taarifa za awali zinaeleza timu zote zinapambana lakini hakuna hata moja iliyowasilisha ofa ya kumsajili. Bouaddi amevutia vigogo wengi kutokana na kipaji kikubwa alichoºnyesha tangu kuanza kwa msimu huu.
Nico Williams
BAYERN Munich inapanga kuwasilisha ombi Athletic Bilbao ili kumsajili Nico Williams, mwenye umri wa miaka 23 dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Awali Nico alikuwa katika rada za Bayern ambayo baada ya kumkosa ndio ikaangukia kwa Luis Diaz. Mkataba wa Nico unatarajiwa kumalizika mwaka 2035. Msimu uliopita alicheza mechi tatu za michuano yote na kutoa asisti mbili.
Malick Fofana
CHELSEA inakumbana na ushindani kutoka Bayern Munich kumwania kiungo wa Olympique Lyon, 20, Malick Fofana. Fofana anaonekana kama mmoja wa vipaji vinavyovutia na klabu kubwa zinammezea mata na Bayern na Chelsea ni miongoni mwa zilizotajwa mara nyingi. Taarifa bado hazijathibitisha ofa rasmi.
Kenan Yıldız
CHELSEA imewatuma skauti wake kumfuatilia mshambuliaji wa Juventus mwenye umri wa miaka 20, Kenan Yıldız, ambaye ni raia wa Uturuki. Kenan Yıldız anaendelea kuonyesha kiwango bora akiwa na Juventus tangu msimu uliopita. Chelsea iliwasilisha ofa ya Euro 65 milioni ili kumsajili lakini ilikataliwa. Mkataba wa sasa wa Yıldız na Juventus unamalizika mwaka 2029.