Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Komenti ya Palmer kwa Mainoo gumzo

Muktasari:

  • Mainoo, 20, aliposti picha zake tano kwenye mtandao wa Instagram ambazo zilikuwa na tafsiri nyingi sana.

LONDON, ENGLAND: STAA wa Chelsea, Cole Palmer amewapagawisha mashabiki kwenye mtandao wa kijamii kutokana na komenti yake aliyotoa kwenye posti ya kiungo wa Manchester United, Kobbie Mainoo huko mtandaoni.

Mainoo, 20, aliposti picha zake tano kwenye mtandao wa Instagram ambazo zilikuwa na tafsiri nyingi sana.

Picha moja alionekana ameketi huku akiwa anatafakari jambo, wakati nyingine imeonyesha akiwa mazoezini, nyingine kwenye gym, zote akiwa mwenyewe na kutuma ujumbe kwamba anajisukuma mwenyewe.

Picha nyingine kwenye posti hiyo ya Mainoo iliyovuta hisia ni ile ya msanii Miles Teller akipiga ngoma kwenye filamu ya Whiplash, inayozungumzia nyota anayeibukia na hapo ndipo palipomfanya Palmer kuweka komenti.

Palmer, 23, alikomenti kwa kusema "3 my boy", akiambatanisha na emoji nyekundu ya moyo, huku ujumbe huko wa Palmer ukiimaanisha ulikuwa na maana  "Jiokoe kijana wangu (aondoke Man United)". Komenti hiyo ilivutia like 10,000 ndani ya saa sita tu za kwanza, ambapo wengi waliamini staa huyo wa Chelsea anamtaka mchezaji mwenzake huyo wa England aondoke Man United.

Mastaa wa Man United, Leny Yoro na Joshua Zirkzee nao walikomenti kwenye posti hiyo ya Mainoo, ambapo wote walikomenti kwa kuweka emoji mjongeo, ambapo Yoro alitumia picha ya Mainoo akishangilia.

Mainoo amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha Man United msimu huu na hilo limemfanya awekwe kando na kocha Thomas Tuchel kwenye timu ya England inayokabiliwa na mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Andorra na Serbia.

Kiungo huyo aliomba kuondoka Man United kwa mkopo kwenye dirisha la majira ya kiangazi, lakini aliambiwa haondoki na anapaswa kupambania namba kwenye kikosi cha Ruben Amorim.

Kiungo huyo Namba 8 hakutumika kwenye mechi mbili za kwanza kwenye Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal na Fulham, kabla ya kucheza kwa dakika 45 kwenye ushindi wa kwanza wa Man United dhidi ya Burnley.

Mainoo sasa anaamini kiwango chake kwenye mechi hiyo kitampa nafasi ya kupangwa na kocha Amorim katika mchezo ujao wa Man United dhidi ya Manchester City utakaopigwa Etihad, Septemba 14.