Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Barcelona amfagilia Rashford

HANS Pict

Muktasari:

  • Rashford aling'ara akiwa Barcelona kwa kufunga mabao 14 na kutoa asisti nyingine 14, huku akiweka wazi kuwa alitamani kuongeza muda wa kuitumikia miamba hiyo ya Hispania.

BRCELONA,HISPANIA: KOCHA wa Barcelona, Hansi Flick, amethibisha kuwa Marcus Rashford hataendelea kubaki Camp Nou baada ya kumaliza kipindi chake cha mkopo, akisema atamkumbuka kutokana na mchango mkubwa alioutoa ndani ya kikosi hicho.

Rashford aling'ara akiwa Barcelona kwa kufunga mabao 14 na kutoa asisti nyingine 14, huku akiweka wazi kuwa alitamani kuongeza muda wa kuitumikia miamba hiyo ya Hispania.

Hata hivyo, matumaini yake yanaonekana kuyeyuka baada ya Barcelona kuwasajili winga Anthony Gordon na Karim Adeyemi kwa jumla ya Pauni 106.5 milioni, hatua inayofanya uwezekano wa klabu hiyo kutumia kipengele cha kumnunua kwa Pauni26 milioni kutoka Manchester United kuwa mdogo.

HAN 01

Kutokana na hali hiyo, Rashford anatarajiwa kurejea Old Trafford, licha ya kuwahi kukiri kuwa alikuwa tayari kuanza maisha mapya nje ya Manchester United. Safari hii, atamkuta kocha mpya Michael Carrick akiwa amepewa jukumu la kuinoa timu hiyo.

Akizungumza kuhusu mshambuliaji huyo, Flick amesema amefurahia kufanya naye kazi na ataikosa huduma yake.

"Ninachoweza kusema kuhusu Marcus nilifurahia sana kufanya kazi naye. Wakati mwingine huwezi kujua kitakachotokea kwa wachezaji waliokuja kwa mkopo.

"Hali yetu haikuwa rahisi, lakini ni mchezaji bora na mtu wa mfano. Ninaamini timu pia itamkosa, nami nitamkosa, lakini hayo ndiyo maisha. Tunapaswa kuyakubali," amesema Flick.

HAN 02

Licha ya Barcelona kupunguza baadhi ya changamoto zake za kifedha baada ya miaka kadhaa ya kubana matumizi, bado klabu hiyo inaendelea kukabiliwa na vikwazo vya matumizi ya fedha.

Mpaka sasa, haijakusanya mapato makubwa kupitia mauzo ya wachezaji, huku pia ikitakiwa kuziba pengo lililoachwa na Robert Lewandowski aliyesajiliwa na Chicago Fire baada ya kumaliza mkataba wake.

Kwa upande wa Rashford, kiwango alichoonyesha msimu uliopita kinatarajiwa kuwavutia klabu kadhaa, hasa baada ya kurejea kwenye kikosi cha England kilichoshiriki Kombe la Dunia.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alifunga bao katika ushindi wa England wa mabao 4-2 dhidi ya Croatia kwenye mechi ya ufunguzi wa Kombe la Dunia, ingawa hakuendelea kung'ara kama ilivyotarajiwa katika mechi zilizofuata.

Rashford bado ana mkataba wa miaka miwili na Manchester United, klabu aliyolelewa tangu akiwa mdogo.

HAN 03

Akizungumza mwezi Mei kuhusu mustakabali wake, Rashford amesema:

"Kama ningekuwa mchawi, ningebaki hapa. Nimekuja kushinda mataji na natamani kushinda mengi iwezekanavyo.

"Hiki ni kikosi bora na naamini kitashinda makombe mengi miaka ijayo. Kuendelea kuwa sehemu ya safari hiyo kungekuwa jambo la kipekee."