Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kombe la Dunia Wanawake 2025 kupigwa England

Muktasari:

  • Tangazo hilo limepokelewa kwa shangwe kubwa, huku likifungua ukurasa mpya wa maendeleo ya soka la wanawake nchini humo.

LONDON, ENGLAND: UINGEREZA na mataifa mengine yamepata heshima ya kuandaa Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake mwaka 2035, ikiwa ni mara ya kwanza kwa michuano hiyo mikubwa kufanyika katika ardhi hiyo tangu Kombe la Dunia la wanaume lilipofanyika mwaka 1966.

Tangazo hilo limepokelewa kwa shangwe kubwa, huku likifungua ukurasa mpya wa maendeleo ya soka la wanawake nchini humo.

Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo, bado kuna changamoto mbalimbali zinazohitaji kushughulikiwa kabla ya kufika mwaka 2035.

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, alizungumza kuhusu ukuaji mkubwa wa soka la wanawake wakati wa hafla ya kutangaza mwenyeji wa michuano hiyo.

Infantino alieleza kuwa Kombe la Dunia la wanawake limepiga hatua kubwa na limeendelea kuwa mashindano yenye mafanikio.

Hata hivyo, uongozi wake bado umekuwa ukikabiliwa na ukosoaji, hasa kutokana na kauli zake za awali kuhusu usawa wa kijinsia na malipo kwa wachezaji wanawake.

Katika Kombe la Dunia la mwaka 2023 lililofanyika Australia na New Zealand, fainali kati ya Hispania na England ilifunikwa kwa kiasi kikubwa na sakata la aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka la Hispania, Luis Rubiales, kumbusu nahodha Jenni Hermoso bila ridhaa yake.

Tukio hilo lilizua maandamano na mjadala mkubwa kuhusu haki na usalama wa wanawake katika soka.

Rubiales baadaye alikutwa na hatia ya kosa la unyanyasaji wa kingono kutokana na tukio hilo.

Kwa sasa, maandalizi ya michuano ya 2035 yanatarajiwa kuhusisha si tu miundombinu na viwanja, bali pia kuboresha mazingira ya soka la wanawake kwa ujumla.

Moja ya changamoto zinazotajwa ni kupungua kwa idadi ya mashabiki wanaohudhuria mechi za Ligi Kuu ya Wanawake England (WSL).

Takwimu zilizotajwa zinaonyesha wastani wa mashabiki katika mechi za wiki nane za mwanzo za msimu wa 2024/25 ulikuwa 8,173, ukashuka hadi 7,472 msimu uliofuata, huku msimu wa sasa ukionyesha mwenendo wa kushuka hadi karibu 5,677.

Hali hiyo imeibua hoja kuhusu namna ya kuongeza mvuto wa ligi hiyo kabla ya kuandaa michuano mikubwa ya dunia.

Changamoto nyingine ni uamuzi wa uwanja utakaotumika kuandaa mchezo wa fainali.

Uwanja wa Wembley unaonekana kuwa chaguo kuu kwa sasa kwa sababu unakidhi masharti yaliyowekwa na FIFA.

Hata hivyo, kuna uwezekano wa uwanja mwingine kupewa nafasi endapo utakamilika na kukidhi vigezo kabla ya mwaka 2035.

Mradi wa Manchester United wa kujenga uwanja mpya wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 100,000 umeingia katika mjadala huo, huku ukitajwa kuwa miongoni mwa viwanja vinavyoweza kuzingatiwa.

Iwapo utateuliwa, Manchester inaweza kuwa mwenyeji wa fainali hiyo, jambo ambalo lingeongeza wigo wa kueneza soka la wanawake nje ya jiji la London.

Kwa ujumla, maandalizi ya Kombe la Dunia 2035 yanatarajiwa kuwa fursa kubwa kwa soka la wanawake nchini Uingereza.

Hata hivyo, mafanikio ya michuano hiyo hayatategemea tu viwanja vikubwa, mapato na idadi ya mashabiki, bali pia namna viongozi watakavyoshughulikia changamoto zilizopo sasa ili kuhakikisha mchezo huo unaendelea kukua katika ngazi zote.