Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha wa Spurs aweka mezani jina la Ivan Toney

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Frank ambaye aliwahi kufanya kazi na Toney walipokuwa Brentford anaamini Spurs inahitaji nguvu zaidi katika eneo la ushambuliaji ili kufanya vizuri msimu huu.

KOCHA wa Tottenham hotspur, Thomas Frank anadaiwa kuwasilisha jina la straika wa Al-Ahli, Ivan Toney kwa mabosi wa Spurs akitaka asajiliwe katika dirisha lijalo la majira ya baridi.

Frank ambaye aliwahi kufanya kazi na Toney walipokuwa Brentford anaamini Spurs inahitaji nguvu zaidi katika eneo la ushambuliaji ili kufanya vizuri msimu huu.

Inaelezwa Toney, 29, ambaye kwa sasa anachota pesa za matajiri wa Saudia anaweza kushawishika kutua Spurs kutokana na heshima kubwa ambayo ipo kati yake na Frank. Akiwa Saudia fundi huyo wa kimataifa wa England ameendelea kuonyesha kiwango bora na msimu huu tayari amefunga mabao 11 katika mechi 15 za michuano yote.

Spurs imekuwa ikipambana kuhakikisha inaziba pengo la Harry Kane kwa muda mrefu lakini haijapata mwenye kiwango hicho.


Declan Rice

ARSENAL inahitaji kiasi kisichopungua Euro 150 milioni ili kumuuza kiungo wa kimataifa wa England, Declan Rice, 26, ambaye Real Madrid imeonyesha nia ya kutaka kumsajili ifikapo mwisho wa msimu huu. Mabosi wa Arsenal hawataki kumuona fundi huyo anaondoka kikosini kwao, lakini wanaweza kufikiria kumwachia ikiwa timu inayomhitaji itaweka mezani ofa inayoanzia kiasi hicho cha pesa.


Sven Botman

MABOSI wa Newcastle United wapo katika mazungumzo na wawakilishi wa beki wao kisiki Mholanzi Sven Botman, 25. Botman amekuwa akiwindwa na vigogo Ulaya na mabosi wa Newcastle wanataka kumsainisha mkataba mpya ili kumuongezea thamani kuja kumuuza kwa bei mbaya, lakini kipaumbele cha kwanza ni kuhakikisha anaendelea kusalia katika kikosi hicho.


Jadon Sancho

BORUSSIA Dortmund ipo katika mazungunzo na Manchester United ili kuipata saini ya winga wa timu hiyo na England, Jadon Sancho ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Aston Villa. Dortmund inataka kumsajili Sancho mwisho wa msimu ikiamini itampata kwa bei chee sababu hayupo katika kiwango bora huko Villa. Sancho aliwahi kuitumikia Dortmund kabla ya kujiunga na Man United ambayo tangu imsajili ameshindwa kufikia matarajio.


Dayot Upamecano

REAL Madrid ina matumaini makubwa ya kumpata beki kisiki wa Bayern Munich, Dayot Upamecano, 27, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo atakuwa mchezaji huru. Awali wababe hao waliripotiwa kuhitaji huduma ya Marc Guehi, lakini mapema wiki hii waliachana na mpango huo kutokana na kiasi kikubwa cha mshahara na bonasi ya usajili anayotaka.


Marc Cucurella

ATLETICO Madrid inamwangalia kwa karibu beki kisiki wa Chelsea, Marc Cucurella, 27, ambaye imepanga kuwasilisha ofa dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Cucurella ni miongoni mwa mastaa tegemeo wa kikosi cha kwanza Chelsea, lakini Atletico inaamini inaweza kumpata ikiwa itawasilisha ofa nono. Staa huyo Mhispania mkataba wake unaisha 2028.


Kobbie Mainoo

CHELSEA, Tottenham Hotspur, Manchester City, Leeds, Everton, Barcelona na Real Madrid zinaripotiwa kuvutiwa na kiungo wa Manchester United, Kobbie Mainoo na zinataka kuwasilisha ofa dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Hivi karibuni Mainoo ambaye hapati nafasi katika kikosi cha Man United amekuwa akihusishwa pia na Napoli ambayo inapambana ili kumpata kwa mkopo wa nusu msimu Januari mwakani.


Nico Paz

CHELSEA imeulizia uwezekano wa kuipata huduma ya kiungo wa Como na timu ya taifa ya Argentina, Nico Paz, 21, lakini inakumbana na upinzani mkali kutoka kwa Real Madrid ambayo pia inahitaji huduma ya staa huyo. Uwezekano wa Chelsea kumpata staa huyo unaonekana kuwa ni mgumu kutokana na uhusiano wa karibu kati ya mchezaji na mabosi wa Madrid kwani kabla ya kutua Como alikuwa akiichezea Real Madrid.