Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

El Clasico yahamia kwa beki wa Borussia Dortmund

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Beki huyo mwenye umri wa miaka 25 kiwango chake kimekuwa matata tangu alipojiunga na Dortmund akitokea Freiburg katika kipindi cha uhamisho wa majira ya kiangazi 2022.

REAL Madrid na Barcelona zimeripotiwa kuhamishia vita ya El Clasico kwenye usajili na miamba hiyo ya LaLiga inachuana vikali katika kuwania saini ya beki wa Borussia Dortmund, Nico Schlotterbeck.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 25 kiwango chake kimekuwa matata tangu alipojiunga na Dortmund akitokea Freiburg katika kipindi cha uhamisho wa majira ya kiangazi 2022.

Schlotterbeck kwa sasa anahesabika kama mchezaji muhimu katika kikosi cha Dortmund, kiasi cha kuvaa kitambaa cha unahodha katika mechi nne zilizopita kwenye ligi.

Hata hivyo, ishu ya beki huyo kudumu Dortmund kwa muda mrefu ndicho kitu cha utata kutokana na miamba hiyo ya Hispania kuingia vitani kumtaka huku mkataba wake ukiwa umebakiza miaka miwili. Ubora wake ndicho kitu kinachofanya miamba ya Ulaya kumhitaji.

Bayern Munich nayo ipo kwenye mchakamchaka huo wa kumsaka beki huyo, sambamba na Liverpool, ambayo inadaiwa kuwa na tatizo katika eneo hilo la uwanja na inamtazama Schlotterbeck kama mtu sahihi wa kuja kuwaokoa.


Elliot Anderson

MANCHESTER United na Newcastle United zinafuatilia kwa karibu maendeleo ya kiungo wa Nottingham Forest na timh ya taifa ya England, Elliot Anderson ambaye zinahitaji kumsajili dirisha lijalo la majira ya baridi. Forest inahitaji ofa kati ya Pauni 100 hadi 120 milioni ili kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 aliyejiunga na Forest akitokea Newcastle United.


Mason Greenwood

BARCELONA inaongoza katika mbio za kuiwania saini ya   mshambuliaji wa zamani wa Manchester United ambaye kwa sasa anaitumikia Olympique Marseille ya Ufaransa. Tottenham Hotspur na West Ham United pia zinafuatilia kwa karibu saini yake. Greenwood, 24, ameonyesha kiwango bora tangu ajiunge na Marseille miaka miwili iliyopita. Tangu kuanza kwa msimu huu amehusika katika mabao 15 ya michuano yote.


Jobe Bellingham

STAA wa Borussia Dortmund, Jobe Bellingham amekataa ofa ya kujiunga na Manchester United iliyodaiwa kutaka kumsajili dirisha lijalo. Taarifa zilidai Man United ilikuwa inaangali uwezekano wa kumchukua kwa mkopo staa huyu mwenye umri wa miaka 20, lakini ripoti zinaeleza amekataa kwani bado anaona anahitaji kukua zaidi kabla ya kujiunga na timu nyingine na kwa maoni yake Dortmund ndiyo timu itakayomfanya akomae.


Joshua Zirkzee

MANCHESTER United imepanga kuzuia maombi yoyote ya uhamisho kutoka kwa klabu zitakazohitaji huduma ya Kiungo wao wa kimataifa wa England, Kobbie Mainoo mwenye umri wa miaka 20 na mshambuliaji wao wa kimataifa wa Uholanzi, Joshua Zirkzee,24, dirisha lijalo. ImefichuKa Man United haitaki kuwauza mastaa hao Januari badala yake wanataka kukaa nao hadi mwisho wa msimu licha ya kuonekana hawapati nafasi ya kutosha kikosi cha kwanza.


Rasmus Hojlund

INAELEZWA Manchester United imeipa Napoli ruhusa ya kumnunua rasmi mshambuliaji wao wa kimataifa wa  Denmark, Rasmus Hojlund, 22, ambaye anacheza katika kikosi chao kwa mkopo. Hojlund alisajiliwa na Napoli dirisha lililopita kwa mkopo wa msimu mmoja lakini katika mkataba wa makubaliano kuna kipengele kinachoiwezesha Napoli kumnunua mazima ikiwa itahitaji kufanya hivyo. Rasmus alijiunga na Man United mwaka 2023 lakini ameshindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa hali iliyosababisha atolewe kwa mkopo mwaka huu.


Alexsandro Ribeiro

WEST Ham United imemweka katika orodha ya mastaa inaowahitaji beki wa Lille na Brazil Alexsandro Ribeiro, 26. Mabosi wa West Ham wapo tayari kutumia zaidi ya Pauni 30 milioni kuhakikisha mchezaji huyu anatua Januari mwakani. West Ham inataka kuimarisha safu yao ya ulinzi baada ya kuwa na changamoto za majeraha hali iliyosababisha ianze vibaya sana msimu huu.


Samu Aghehowa

ARSENAL imeingia katika vita dhidi ya Tottenham na Newcastle ili kuipaa saini ya straika wa FC Porto,   Samu Aghehowa,21. Staa huyu pia anacheza timu za vijana za Hispania amezivutia timu nyingi kutokana na kiwango alichoonyesha tangu msimu uliopita. Spurs ndiyo ilikuwa ya kwanza kuhusishwa naye lakini sasa inakumbana na upinzani wa kutosha kutoka kwa Arsenal na Newcastle ambazo zipo tayari kulipa takriban Pauni 50 milioni ili kumpata staa huyu.