Kocha Man United atoa msisitizo, asema hauzwi mtu
Muktasari:
- Kocha Mreno, Amorim amesema hawezi kuruhusu kumpoteza mchezaji kama Kobbie Mainoo katika kipindi kama hiki cha msimu, ambapo kikosi kitahitaji kuwa na watu kwa ajili ya kumaliza ligi vizuri.
MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA Mkuu wa Manchester United, Ruben Amorim amesema hakuna mchezaji atakayeuzwa kwenye dirisha la Januari kama hatakuwa amepatikana mbadala wake.
Kocha Mreno, Amorim amesema hawezi kuruhusu kumpoteza mchezaji kama Kobbie Mainoo katika kipindi kama hiki cha msimu, ambapo kikosi kitahitaji kuwa na watu kwa ajili ya kumaliza ligi vizuri.
Amesema: "Itakuwa ngumu kwa mtu kuondoka kama klabu haitakuwa imepata mchezaji wa kuja kuchukua nafasi yake.
"Tuna wachezaji wachache. Hata kama tungekuwa na kikosi chote, bado tungekuwa na mazingatio ya kile kinachoweza kutokea. Hii ni klabu yenye mipango mikubwa. Tunapambana na mambo ya vyombo vya habari na tunahitaji kushinda kila mechi. Haijalishi kitu, hakuna kisingizio."
Amorim aliongeza: "Tupo kwenye wakati mgumu kwa sasa, lakini klabu ina mipango na tutaendelea kusimamia mipango yetu.
"Kama tutapata nafasi ya kuleta mchezaji, basi tutafanya hivyo kwa ajili ya faida ya klabu. Kama tutashindwa, basi tunao Jack (Fletcher), tunaye Shea (Lacey) na baada ya wiki tatu, tutakuwa na Amad, Noussair (Mazraoui) na Bryan (Mbeumo), pamoja na kurejea kwa Bruno (Fernandes) na Kobbie Mainoo."