Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Uefa, Paris yazidi kukumbwa na vurugu

PARIS Pict

Muktasari:

  • Polisi waliokuwa wamebeba virungu na ngao walionekana wakisambaratisha umati wa mashabiki  uliokuwa kwenye eneo la Champs-Elysees ambao uligeuza sherehe hizo kuwa sehemu ya machafuko.

PARIS, UFARANSA: JIJI la Paris limejikuta kwenye vurugu kwa siku mbili mfululizo baada ya kuzuka kwa sintofahamu katika siku ya pili kufuatia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati PSG ilipokuwa ikitembeza kombe mitaani.

Polisi waliokuwa wamebeba virungu na ngao walionekana wakisambaratisha umati wa mashabiki  uliokuwa kwenye eneo la Champs-Elysees ambao uligeuza sherehe hizo kuwa sehemu ya machafuko.

Shangwe zilizojaa furaha baada ya PSG kuichakaza Inter Milan kwa mabao 5-0 kwenye fainali mjini Munich, Jumamosi, ziliendelea Jumapili nchini Ufaransa. Hata hivyo, furaha iligeuka giza baada ya machafuko kuripotiwa.

Mashabiki wa PSG walikumbana na gesi ya kutoa machozi usiku kucha kufuatia mapambano yaliyosababisha vifo vya watu wawili na kujeruhiwa karibu watu 200 Jumamosi.

Zaidi ya watu 600 walikamatwa kufuatia vurugu hizo, huku magari, mapipa ya taka na magodoro yakichomwa moto.

Siku moja baada ya vurugu za awali, hali ya sintofahamu ilizidi pale polisi walipokabiliana tena na mashabiki waliokuwa wamekusanyika kwa sherehe rasmi za ushindi. Wachezaji na benchi la ufundi la PSG waliungana na mashabiki 110,000 kwenye gwaride la ushindi lililofanyika Champs-Elysees juzi, Jumapili, mchana.

Mashabiki walijaribu kujazana kwenye mitaa ya jiji hilo kushuhudia gwaride hilo, lakini kwa muda mfupi tu idadi ya watu ilizidi uwezo wa eneo na kusababisha msongamano na hatimaye vurugu.

Polisi wa kutuliza ghasia walionekana wakijaribu kuwatawanya mashabiki kwa kuwafukuza kwenda mitaani. Video zilizosambazwa mtandaoni zinaonyesha askari wakikimbia kwa kasi juu ya daraja la Alma kuelekea kwenye kundi la mashabiki. Moshi mzito wa bluu kutoka kwenye baruti za sherehe ulionekana karibu na Mnara wa Eiffel.

Ofisa mmoja wa serikali alisema: “Wanatutupia kila kitu walichonacho.”

Polisi walilazimika kutumia silaha za risasi za mpira ili kuwatawanya mashabiki  waliokuwa wameshika silaha kama vile fimbo ndefu za chuma na matofali.

Machafuko hayo yamejiri baada ya vifo viwili kuthibitishwa kufuatia ghasia zilizotokea baada ya PSG kutawazwa mabingwa wa Ulaya katika tukio lililoushangaza ulimwengu wa soka.

Tukio baya zaidi lilitokea Dax, kusini-magharibi mwa Ufaransa ambako kijana mwenye umri wa miaka 17 alichomwa kisu tumboni. Msemaji wa polisi alisema: “Alikuwa sehemu ya umati uliokuwa ukisherehekea ushindi wa PSG katika eneo maalumu la mashabiki, na alifariki dunia hospitali kutokana na majeraha yake.”

Pia mtu mmoja aliuawa baada ya pikipiki yake kugongana na gari jijini Paris.

Sherehe hizo zilizotarajiwa kuwa za kihistoria zimegeuka kuwa kipindi cha huzuni, hasira na machafuko zikiutia doa ushindi mkubwa wa PSG wa mabao 5-0.