Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Karetsas aanguka uwanjani, awahishwa hospitali baada ya kuzimia

Muktasari:

  • Borussia Dortmund ilieleza kuwa Karetsas alipata “tatizo la mzunguko wa damu”, ambapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Ugiriki alianguka bila kuguswa na mchezaji wa timu pinzani na kisha akakaa kwenye nyasi.

DORTMUND, UJERUMANI: KIUNGO wa Borussia Dortmund, Konstantinos Karetsas, 18, alilazimika kuwahishwa hospitali baada ya kuanguka uwanjani katika kipindi cha kwanza cha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Villarreal na hadi jana alikuwa akifanyiwa uchunguzi mkali wa kitabibu kubaini tatizo.

Borussia Dortmund ilieleza kuwa Karetsas alipata “tatizo la mzunguko wa damu”, ambapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Ugiriki alianguka bila kuguswa na mchezaji wa timu pinzani na kisha akakaa kwenye nyasi.

Alitoa ishara kuomba msaada wa kitabibu, licha ya kwamba muda mfupi kabla ya tukio hilo alikuwa akidhibiti mpira, akipiga chenga na kutoa pasi bila kuonekana kuwa na tatizo lolote.

Karetsas, aliyejiunga na Dortmund akitokea KR Genk katika usajili wa dirisha kubwa lililopita alikuwa akicheza mechi yake ya tano tangu ajiunge na klabu hiyo. Tukio hilo liliibua hofu, lakini Dortmund ilieleza kuwa hali yake inaendelea vizuri kadri inavyotarajiwa.

Katika taarifa, Dortmund ilisema: “Konstantinos Karetsas alilazimika kuondoka uwanjani katika mchezo dhidi ya Villarreal kutokana na matatizo ya mzunguko wa damu. Kosta anaendelea vizuri kadiri inavyotarajiwa kutokana na mazingira yaliyotokea, na anafanyiwa uchunguzi zaidi.”

Kulikuwa na wasiwasi mkubwa kwenye benchi la Dortmund, huku nyota wa zamani wa klabu hiyo, Mats Hummels, ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka akieleza hofu yake akisema: “Madaktari walipoacha kabisa kuangalia miguu yake na kuelekeza nguvu zao kwenye sehemu ya juu ya mwili wake pekee, nilihisi hofu kubwa sana.

“Hatungependa kumuona mtu yeyote akipitia hali kama hiyo. Haya yanakuwa matukio ya kutisha sana ambayo tunalazimika kuyaona.”

Karetsas alibadilishwa na Ethan Nwaneri, anayekipiga Dortmund kwa mkopo kutoka Arsenal, dakika ya 27 ya mchezo huo ambao ilishinda kwa mabao 3-2.