Jose Mourinho awavuruga mashabiki Real Madrid
Muktasari:
- Kocha huyo aliyerejea kuiongoza Madrid alianza vyema kwenye mchezo wake wa kwanza wa ushindani Jumamosi usiku, baada ya timu yake kupata bao la kuongoza mapema dhidi ya Espanyol.
MADRID, HISPANIA: KOCHA Jose Mourinho alihitaji dakika 15, pekee kuwafanya mashabiki wa Real Madrid kuanza kuamini tena uwezo wake, lakini mambo yalibadilika haraka baada ya timu hiyo kushindwa kuendeleza kiwango chake katika mechi dhidi ya Espanyol ya ushindi wa mabao 2-1.
Kocha huyo aliyerejea kuiongoza Madrid alianza vyema kwenye mchezo wake wa kwanza wa ushindani Jumamosi usiku, baada ya timu yake kupata bao la kuongoza mapema dhidi ya Espanyol.
Mourinho, aliyerejea LaLiga baada ya miaka 13, aliweka kikosi kilichokuwa na mtazamo wa kushambulia, huku Madrid ikiwafuata wapinzani wake kwa kasi.
Katika mchezo huo, Jude Bellingham na Arda Guler waliungana na Kylian Mbappe pamoja na Vinicius Jr katika safu ya mbele, huku Bernardo Silva akicheza nafasi ya kiungo wa chini pamoja na Fede Valverde.
Vinicius naye ameongeza nguvu katika presha kutoka eneo la mbele, jambo lililoifanya Madrid kuonekana kuwa na kasi kubwa katika dakika za mwanzo.
Guler, ambaye alipitia kipindi cha kupanda na kushuka chini ya makocha Xabi Alonso na Alvaro Arbeloa, alitoa pasi ya mwisho iliyomuwezesha Bellingham kufunga baada ya dakika tisa pekee.
Madrid iliendelea kupiga pasi kwa kasi na kwa lengo, huku wachezaji wake wakisukuma mashambulizi mbele na kuwafanya wapinzani wao kujilinda.
Vinicius, ambaye Arsenal ilikuwa ikimuwania kabla ya kusaini mkataba mpya na Madrid, alionyesha pia uwezo kubwa katika kukimbia bila mpira.
Bellingham, nyota wa England katika Kombe la Dunia, alisifiwa na baadhi ya mashabiki kwenye mitandao ya kijamii kwa kuonyesha kiwango kilichofanana na kile cha kiungo wa zamani wa England, Frank Lampard, wa mwaka 2005.
Shabiki mmoja aliandika: “Ni mwanzo unaotia matumaini wa Mourinho Ball.”
Mourinho pia alionyesha baadhi ya tabia zake za zamani, akitoka kwenye benchi kwenda kumlalamikia mwamuzi katika tukio moja.
Kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya mashabiki waanze tena kumtaja kama mmoja wa makocha bora zaidi.
Hata hivyo, mambo yalianza kubadilika.
Madrid ilienda mapumziko ikiwa sare, hali iliyofanya maoni ya mashabiki kuanza kubadilika.
Kisha timu hiyo ikaruhusu bao kutokana na uzembe mkubwa wa kiulinzi, huku baadhi ya mashabiki wakidai kuwa udhaifu ulioonekana katika timu za Mourinho katika miaka ya karibuni ulianza kujitokeza.
Baadhi yao hata walianza kutabiri mapema kuwa Mourinho huenda asidumu kwa muda mrefu katika kibarua hicho.
Mtumiaji mmoja wa X aliandika kwa kejeli: “Kamanda Mkuu Jose Mourinho, siku zako zinahesabika.”