Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ISHOWSPEED: Shabiki wa Ronaldo anayepiga pesa mtandaoni

ATM Pict

Muktasari:

  • Mbali ya utajiri ambao ameupata kupitia madili mbalimbali, mashabiki wake pia wamekuwa wakifaidika kupitia jina lake.

CINCINNATI, MAREKANI: HIVI karibuni Cristiano Ronaldo alitangazwa kuwa mchezaji wa kwanza anayecheza soka kufikisha utajiri wa Dola 1 bilioni.

Mbali ya utajiri ambao ameupata kupitia madili mbalimbali, mashabiki wake pia wamekuwa wakifaidika kupitia jina lake.

Miongoni mwa mashabiki wake ambao wamepata utajiri na umaarufu kupitia jina lake ni Darren Watkins Jr, anayefahamika zaidi kwa jina la IShowSpeed.

Kijana huyu kutoka Cincinnati, Marekani, amepata sana umaarufu katika mitandao ya kijamii hasa baada ya kuwa anaigiza staili ya ushangiliaji wa Ronaldo na kutembelea katika mechi ambazo staa huyu anacheza. Leo tumekusogezea jinsi anavyopiga pesa na utajiri wake kwa ujumla.

AT 05

JINSI SPEED ANAVYOPIGA PESA

Speed alianza kupanda chati mwaka 2020 kupitia michezo ya Fortnite na FIFA, lakini umaarufu wake ulilipuka zaidi baada ya kuanza kufanya live-streaming.

Kwa sasa, asilimia kubwa ya utajiri wake unatokana na pesa anazoingiza kupitia YouTube ambako ana wafuasi zaidi ya wafuasi milioni 44 na hupata zaidi ya Dola 500,000  kwa mwezi kupitia mapato ya mtandao huo.

Staa huyu pia hutumia TikTok na Instagram kama sehemu ya kujipatia pesa ambapo mitandao hiyo inamlipa kwa matangazo, pia baadhi ya kampuni kama Prime Energy Drink hutoa pesa ili kuwatangazia vinywaji vyao katika kurasa zake.

Speed pia ni balozi wa kampuni kama Adidas, Rumble, na Kick Live.

Staa huyu pia anapiga pesa kupitia biashara yake ya uuzaji wa  nguo na vifaa vya mashabiki inayoitwa --SpeedGang’.

Kwa wastani, inakadiriwa Speed huingiza zaidi ya Dola 10 milioni kwa mwaka kutokana na shughuli hizi. Kiujumla utajiri wake unafikia Dola 30 milioni.

AT 03

 NYUMBA

Kutokana na mafanikio yake makubwa, Speed amenunua nyumba kadhaa nchini Marekani.

Nyumba yake ya kifahari huko Los Angeles inakadiriwa kuwa na thamani ya Dola milioni 3, ikiwa na studio ya kisasa kwa ajili ya kurusha livestreams, gym binafsi, na bwawa la kuogelea.

Aidha, inasemekana ana nyumba nyingine ndogo kwa ajili ya familia yake mjini Cincinnati, Ohio, ambayo alinunua mwaka 2022 kwa Dola 2 milioni.

AT 04

SAFARI NA NDEGE

Licha ya kwamba hana ndege binafsi, mara nyingi husafiri kwa ndege binafsi za kukodi kwenda kushuhudia mechi za Cristiano Ronaldo au hafla za FIFA.

Safari yake maarufu zaidi ni ile ya kwenda Qatar mwaka 2022, ambayo alihudhuria Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza na akazidi kuwa maarufu.

AT 02

 MISAADA KWA JAMII

IShowSpeed amekuwa akionyesha moyo wa kusaidia sana. Mwaka 2024 alitoa Dola 250,000 kusaidia waathirika wa mafuriko nchini Nigeria na kisha kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwa watoto wa shule nchini Ureno alipokwenda kumuona Ronaldo.

Pia amezindua mfuko uitwao Speed Foundation, unaolenga kusaidia vijana wanaotaka kuwa content creators lakini hawana vifaa.

AT 01

 MAISHA NA BATA

Speed ni shabiki mkubwa wa Cristiano Ronaldo, jambo lililomfanya kupata umaarufu zaidi.

Hata hivyo, mbali na kelele na utani wake, Speed ni kijana mwenye malengo makubwa  amekiri mara kadhaa kuwa anataka kuwa mwanamuziki na mfanyabiashara mkubwa.

Amerekodi nyimbo kadhaa kama ‘World Cup’ na ‘Shake’€ambazo zimetazamwa zaidi ya mara milioni 200 kwenye YouTube. Tangu mwezi uliopita Speed ameripotiwa kuwa katika uhusiano na mrembo, Marwa.