Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isak aanza kulipa Liverpool

LIVERPOOL Pict

Muktasari:

  • Isak alitua Anfield kwa kishindo kikubwa, lakini mwanzo mgumu na jeraha la kuvunjika mguu alilopata Desemba vilifanya msimu wake wa kwanza Liverpool kuwa wa kusikitisha. Alifunga mabao manne pekee katika mechi 22.

LONDON, ENGLAND: IMECHUKUA muda, lakini mshambuliaji wa Liverpool, Alexander Isak, ameanza kuonyesha thamani ya fedha zilizotumika kumsajili kutoka Newcastle United kwa ada ya rekodi ya Uingereza ya pauni 125 milioni, Agosti 2025.

Isak alitua Anfield kwa kishindo kikubwa, lakini mwanzo mgumu na jeraha la kuvunjika mguu alilopata Desemba vilifanya msimu wake wa kwanza Liverpool kuwa wa kusikitisha. Alifunga mabao manne pekee katika mechi 22.

Msimu huu mambo yamebadilika. Bao lake dhidi ya Brighton Jumapili liliisaidia Liverpool kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu iliyokuwa katika kiwango bora kwenye Ligi Kuu England, na kumfikisha kwenye mabao sita katika kampeni hii.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akifunga kwa wastani unaokaribia bao moja kwa kila mchezo, huku akifunga zaidi ya nusu ya mabao yote ya Liverpool katika Ligi Kuu msimu huu.

LIVER 01

Kama ilivyokuwa katika mchezo uliopita dhidi ya Brentford, Isak hakucheza kwa kiwango cha kuvutia kila dakika, lakini alifunga bao muhimu lililoipa Liverpool nafasi ya kutulia. Bao hilo liliiweka timu yake katika nafasi nzuri dhidi ya Brighton, iliyotawala umiliki wa mpira kwa asilimia 64 na kumaliza mchezo ikiwa na takwimu bora zaidi za nafasi za kufunga mabao zinazotarajiwa (xG) kuliko Bournemouth ya Andoni Iraola.

Liverpool ilidhibiti mchezo hadi mwisho, katika kile kilichoweza kuwa mojawapo ya maonyesho yake bora zaidi kwenye ligi chini ya Iraola. Kocha huyo alipata ushindi wake wa kwanza wa ligi akiwa Anfield, katika jaribio lake la nne.

Isak amefunga mabao mengi ya Ligi Kuu msimu huu kuliko wachezaji wote isipokuwa Erling Haaland wa Manchester City, ambaye ana mabao tisa. Hayo ndiyo makali ambayo Liverpool ilitarajia kuyaona ilipomsajili kutoka Newcastle.

Wakati Isak akipambana na majeraha katika msimu wa 2025/26, ndani ya klabu kulikuwa na imani kuwa alikuwa mchezaji wa muda mrefu na kwamba tathmini ya kweli ya uwezo wake ingefanyika baada ya kurejea katika utimamu kamili. Kwa kuzingatia kiwango chake cha hivi karibuni, uvumilivu huo unaonekana kuanza kuzaa matunda.

LIVER 02

“Leo tulicheza vizuri sana dhidi ya timu nzuri,” amesema Isak. “Kipindi cha kwanza ndicho hasa tunachotaka kukiona kutoka kwetu, kushinda mipira na kucheza kwa kasi na nguvu.”

Kinachotia matumaini kwa Iraola na Liverpool ni kwamba Isak bado hajafikia kiwango chake cha juu. Hilo linaweza kuwa onyo kwa wapinzani wao katika Ligi Kuu, huku Arsenal ikiwa mpinzani wao anayefuata kwenye ligi.

“Ikiwa Alex Isak atapata nafasi hizo na tukampelekea krosi nzuri, anaweza kuwa tishio. Katika tukio hili, Barcola alishinda pambano la mpira na kuwahi mpinzani, akituwezesha kufika katika nafasi hiyo,” amesema Iraola.

Ushindi huo ulikuwa wa nne mfululizo kwa Iraola tangu Liverpool ilipopoteza dhidi ya Manchester City Anfield wiki mbili zilizopita.

Mashabiki waliojitokeza licha ya hali mbaya ya hewa iliyofuatia Dhoruba ya Boelo walishuhudia Liverpool ikianza kwa kasi na kucheza vizuri katika ulinzi, ikiizuia Brighton iliyokuwa imefunga mabao 15 katika mechi zake nne zilizotangulia za ligi.

Mbali na nafasi ya mapema ya Yasin Ayari, aliyepiga shuti lililopaa juu ya lango, kikosi cha Fabian Hürzeler hakikupata nafasi nyingi za wazi.

Ronald Araujo aliendelea kuonyesha kiwango bora, huku safu ya ulinzi ya Liverpool ikipata mchezo wake wa nne bila kuruhusu bao katika mechi nane za ligi msimu huu.

Kwa upande mwingine, Liverpool ilimiliki mpira kwa asilimia 35.6 pekee. Hiyo ilikuwa rekodi yake ya pili ya chini zaidi ya umiliki wa mpira katika ushindi wa nyumbani wa Ligi Kuu tangu takwimu hizo zilipoanza kurekodiwa msimu wa 2003/04.