Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hossam: Misri haimtegemei Salah

HOSSAM Pict

Muktasari:

  • Kauli hiyo imekuja baada ya Hassan hivi karibuni kuvuta hisia kutokana na matamshi makali aliyotoa kuhusu baadhi ya wachezaji wa timu hiyo pamoja na kiwango cha Ligi Kuu ya Misri.

CAIRO, MISRI: KOCHA wa timu ya taifa ya Misri, Hossam Hassan, amesema kikosi chake hakiwezi kumtegemea nyota Mohamed Salah kuelekea mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Afrika Kusini 'Bafana Bafana'.

Kauli hiyo imekuja baada ya Hassan hivi karibuni kuvuta hisia kutokana na matamshi makali aliyotoa kuhusu baadhi ya wachezaji wa timu hiyo pamoja na kiwango cha Ligi Kuu ya Misri.

Taarifa zilidai kauli hizo zilisababisha mvutano kati ya kocha huyo na baadhi ya wachezaji, akiwamo Salah.

Salah hakuwamo kwenye kikosi cha Misri kilichoitandika Sudan Kusini mabao 5-0 Jumanne iliyopita katika mchezo wa pili wa kampeni yao ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Misri sasa inatarajiwa kuvaana na Bafana Bafana Jumapili katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

HOSSA 01

Akizungumza baada ya ushindi huo dhidi ya Sudan Kusini, Hassan amesema uwepo wa Salah ni muhimu, lakini timu hiyo haiwezi kujengwa na kumtegemea mchezaji mmoja.

“Salah ni mchezaji muhimu sana katika soka la dunia wakati wowote, lakini hakuwapo kutokana na sababu binafsi,” amesema Hassan.

“Ndiyo maana nasema timu nzima ya taifa ilikuwa inapitia mazingira magumu katika mchezo dhidi ya Angola. Mambo yangekuwa tofauti kama tungekuwa na muda mrefu zaidi wa maandalizi na kama tungeepuka majeraha.

“Sitoi visingizio wala sababu za kujitetea kwa sababu timu ya taifa inaweza kuathirika, lakini haimtegemei mchezaji mmoja. Wachezaji wote ni muhimu.

HOSSA 02

“Wakati huo huo, si sahihi kwa nchi yenye watu milioni 120 kuifanya timu ya taifa imtegemee mchezaji mmoja.

“Ni jukumu langu kufanya kazi na wachezaji walio tayari na waliopo ili kujenga msingi imara wa timu ya taifa.

“Huenda nikachagua maneno yangu kwa umakini ninapozungumza kwa sababu nia yangu ni nzuri, lakini mara nyingi sieleweki,” amesema Hassan.