Hizi hapa dabi hamsini EPL 2025/26
Muktasari:
- Katika kujiandaa na mechi ngumu za aina kama hiyo, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amejiandaa kufanya usajili wa nguvu ikiwamo kusaka mastraika wa viwango vya dunia, akiwamo Alexander Isak wa Newcastle United, Viktor Gyokeres wa Sporting CP, Benjamin Sesko wa RB Leipzig na Ollie Watkins wa Aston Villa.
LONDON, ENGLAND: MKEKA wa ratiba ya Ligi Kuu England umeshawekwa hadharani, ambapo sasa mikikimikiki hiyo itaanza rasmi, Ijumaa ya Agosti 15, wakati mabingwa watetezi Liverpool watakaporusha kete yao ya kwanza dhidi ya Bournemouth uwanjani Anfield.
Lakini, gumzo kubwa la ratiba hiyo ya Ligi Kuu England iliyotangazwa Jumatano iliyopita ni mechi ya Manchester United na Arsenal itakayopigwa kwenye wiki ya kwanza ya michuano hiyo. Kipute hicho kitapigwa Jumapili ya Agosti 17.
Katika kujiandaa na mechi ngumu za aina kama hiyo, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amejiandaa kufanya usajili wa nguvu ikiwamo kusaka mastraika wa viwango vya dunia, akiwamo Alexander Isak wa Newcastle United, Viktor Gyokeres wa Sporting CP, Benjamin Sesko wa RB Leipzig na Ollie Watkins wa Aston Villa.
Hata hivyo, mashabiki wa ligi hiyo wanachowaza ni kuhusu mechi za dabi, zinapigwa lini? Kwa maelezo tu, kutakuwa na jumla ya mechi 50 kati ya 380 za EPL msimu wa 2025/26 ambazo zitakuwa za dabi baada ya ratiba hiyo iliyotolewa Jumatano.
Dabi ni mechi inayohusu timu mbili zinazotokea kwenye eneo moja kijiografia, kwamba timu za jiji moja au timu zenye upinzani mkali na kuhesabika kama mahasimu wakubwa.
Dabi nyingine zinakuwa za kihistoria tu kama ile ya Crystal Palace ya London na Brighton ya Sussex, ambayo mechi yao imekuwa ikihesabika kama dabi, kwa sababu timu hizo zilikutana mara nyingi miaka ya 1970, ikiwamo mechi tano msimu wa 1976/77. Timu hizo zimetengananishwa na barabara ya M23.
London derby
Agosti 17: Chelsea v Crystal Palace
Agosti 23: West Ham v Chelsea
Agosti 30: Chelsea v Fulham
Septemba 13: Brentford v Chelsea, West Ham v Tottenham
Septemba 20: Fulham v Brentford, West Ham v Crystal Palace
Oktoba 4: Arsenal v West Ham
Oktoba 18: Fulham v Arsenal, West Ham v Brentford
Oktoba 25: Arsenal v Crystal Palace
Novemba 1: Crystal Palace v Brentford, Tottenham v Chelsea
Novemba 22: Arsenal v Tottenham
Novemba 29: Chelsea v Arsenal, Tottenham v Fulham
Desemba 3: Arsenal v Brentford
Desemba 6: Fulham v Crystal Palace, Tottenham v Brentford
Desemba 27: Crystal Palace v Tottenham, West Ham v Fulham
Desemba 30: Brentford v Tottenham, Crystal Palace v Fulham
Januari 7: Fulham v Chelsea
Januari 17: Chelsea v Brentford, Tottenham v West Ham
Januari 24: Crystal Palace v Chelsea
Januari 31: Chelsea v West Ham
Februari 11: Brentford v Arsenal
Februari 21: Tottenham v Arsenal
Februari 28: Arsenal v Chelsea, Fulham v Tottenham
Machi 4: Fulham v West Ham, Tottenham v Crystal Palace
Aprili 18: Brentford v Fulham, Crystal Palace v West Ham
Mei 2: Arsenal v Fulham, Brentford v West Ham
Mei 9: West Ham v Arsenal
Mei 17: Brentford v Crystal Palace, Chelsea v Tottenham
Mei 24: Crystal Palace v Arsenal
Hizi hapa dabi 50 zitakazopigwa kwenye Ligi Kuu England msimu wa 2025/26
Manchester derby
Septemba 13: Man City v Man Utd
Januari 17: Man Utd v Man City
Merseyside derby
Septemba 20: Liverpool v Everton
Aprili 18: Everton v Liverpool
Tyne-Wear derby
Desemba 13: Sunderland v Newcastle
Machi 21: Newcastle v Sunderland
M23 derby
Novemba 8: Crystal Palace v Brighton
Februari 7: Brighton v Crystal Palace