Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii hapa dawa ya kuitibu Man United

DAWA Pict

Muktasari:

  • Mechi mbili bila ushindi katika msimu mpya huku takwimu zikisoma vibaya kwa kocha Ruben Amorim kiasi kwamba gwiji wa klabu hiyo, Wayne Rooney akianza kuonyesha wasiwasi. Kocha Amorim amevuna pointi 28 tu katika mechi 29 alizocheza kwenye Ligi Kuu England, hivyo anahitaji kubadili mambo kwa haraka kabla ya ajira haijafa.

MANCHESTER, ENGLAND: BAADA ya kuonekana kama timu imerudi kwenye ubora wake dhidi ya Arsenal, Manchester United imebofya kitufe cha ‘factory reset’ na kurudi kulekule kwa kile ilichokifanya kwa  Fulham.

Na sasa mashabiki wa timu piznani wanaaambia “watashuka daraja” ikiwa ni maneno ya kejeli dhidi yao.

Mechi mbili bila ushindi katika msimu mpya huku takwimu zikisoma vibaya kwa kocha Ruben Amorim kiasi kwamba gwiji wa klabu hiyo, Wayne Rooney akianza kuonyesha wasiwasi. Kocha Amorim amevuna pointi 28 tu katika mechi 29 alizocheza kwenye Ligi Kuu England, hivyo anahitaji kubadili mambo kwa haraka kabla ya ajira haijafa.

Wastani wake wa ushindi kwenye ligi ni asilimia 24.7 tu huku mechi zijazo ni Manchester City,  Chelsea na Brentford, hivyo unaweza kuona uhakika wa kushinda ulivyofinyu. Msimu uliopita ulikuwa mgumu, hivyo kocha Amorim alibeba matumaini ya kufanya vizuri msimu huu. Lakini, mwanzo umekuwa mgumu, mechi mbili pointi moja na kiwango kinashtua. Kutokana na hilo, kocha Amorim anapaswa kufanya mambo manne kama anataka kunusuru ajira yake.

1.Anyumbulike: Mfumo wa 3-4-2-1 ulifanya kazi Sporting Lisbon, lakini umegoma Old Trafford. Man United haionekani kuwa na wachezaji wa kufiti kwenye mtindo huo wa kiuchezaji. Hilo linamsukumu Amorim anyumbulike, atafuta staili nyingine ya kiuchezaji na si kung’ang’ania 3-4-2-1. Anapaswa kutafuta mfumo ambao atapata huduma bora kutoka kwa wachezaji wake kama Bruno Fernandes, ambaye anafiti Namba 10 kuliko Namba 6.

3-4-2-1 inamnyima uhuru winga Amad Diallo na kuwafanya Bryan Mbeumo na Matheus Cunha kushindwa kung’ara ipasavyo. Atumie 4-2-3-1 au 4-3-3.

2.Apange straika: Man United inahitaji mabao na Amorim anapuuza kumchezesha straika. Baada ya kutumia zaidi ya Pauni 200 milioni kwenye dirisha hili kunasa safu mpya ya ushambuliaji, Man United bado imeshindwa kufunga bao la kitimu msimu huu. Bao moja ililonalo hadi sasa ni la beki Rodrigo Muniz wa Fulham kujifunga. Kocha mwenzake wa Arsenal, Mikel Arteta hakutaka kupoteza muda kumtumia straika wake, Viktor Gyokeres, ambaye alifunga mara mbili kwenye ushindi wa 5-0 dhidi ya Leeds. Lakini, Amorim alimweka benchi straika wake wa Pauni 74, Benjamin Sesko kwenye mechi ya pili mfululizo ili tu ampange Mason Mount huku akimweka nje pia straika Rasmus Hojlund. Cunha, ambaye ni mahiri zaidi anapocheza wingi ya kushoto au Namba 10, ndiye anayepangwa kama straika.

3.Asajili kipa: Amorim anahitaji kusajili kipa mpya kabla ya dirisha halijafungwa Jumatatu ijayo. Klabu ilipata kuwa na makipa mahiri kabisa kama Peter Schmeichel na Edwin van der Sar sasa ina makipa wa viwango duni. Amorim ameamua kumtumia kipa namba mbili, Altay Bayindir hata baada ya kufanya makosa dhidi ya Arsenal, hiyo ilionyesha hana  imani na Andre Onana. Mabeki wa Man United kwa sasa wanacheza wakiwa na mashaka makubwa kutokana na uwezo wa kipa wao.

4.Kuongeza wabunifu kwenye kiungo: Safu ya kiungo ya Man United ilikuwa kwenye majanga makubwa dhidi ya Fulham kwenye kipindi cha pili. Baada ya kuongoza 1-0, Amorim imeshindwa kutengeneza nafasi katikati ya uwanja na kuwapa nafasi viungo wa Fulham kutawala eneo hilo la kati ya uwanja. Amorim alimwaanzisha Casemiro, 33 na Fernandes na Mainoo aliishia tu kukaa benchi. Baadaye aliingizwa Manuel Ugarte na timu iliendelea kukosa ubinifu kwenye eneo la kiungo huku Fernandes akishindwa kumkaba Emile Smith Rowe, aliyekwenda kufunga bao la kusawazisha la Fulham. Amorim anahitaji kuwapa nafasi viungo wenye ubunifu kama Mainoo ili kuokoa jahazi.