Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Heat wamzunguke Giannis, Adebayo mipira ya alama 3?

Muktasari:

  • Katika kipindi cha mapumziko ya NBA, timu nyingi kwa kawaida huwa zimekamilisha kazi za vikosi vyao na kujikuta zikiwa tayari kwa msimu mpya. Hata hivyo, hiki hakijawa kipindi cha kawaida cha mapumziko kwa Miami Heat.

MIAMI, MAREKANI: MIAMI Heat ya sura mpya ina supastaa wa kikapu Giannis Antetokounmpo pamoja na Bam Adebayo. Kwa pamoja wanahitaji nini zaidi ili kushindana katika Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), Kanda ya Mashariki?

Katika kipindi cha mapumziko ya NBA, timu nyingi kwa kawaida huwa zimekamilisha kazi za vikosi vyao na kujikuta zikiwa tayari kwa msimu mpya. Hata hivyo, hiki hakijawa kipindi cha kawaida cha mapumziko kwa Miami Heat.

Timu hiyo ilibadilishana wachezaji wanne na machaguo matatu ya raundi ya kwanza (pamoja na kubadilishana chaguo la raundi ya kwanza na  la raundi ya pili), ili kumnyakua Giannis Antetokounmpo, MVP wa NBA mara mbili kutoka Milwaukee Bucks mwishoni mwa Juni. Kisha, Heat ilijaribu kumshawishi LeBron James, MVP wa NBA mara nne kurejesha sura yake mara ya mwisho, lakini ikaishia kumshuhudia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41 akisaini Philadelphia 76ers wiki tatu baada tu ya kuanza kwa Julai.

Na sasa, ikiwa imesalia chini ya miezi miwili kabla ya kuanza kwa kambi ya mazoezi, Heat ina nafasi tatu zilizo wazi kwenye kikosi na maswali ambayo bado hayajajibiwa.


ISHU YA MASHAMBULIZI

Kiwango cha juu cha Miami na uwezo wake wa kushindania ubingwa katika Ukanda wa Mashariki huenda ukategemea ulinzi. Hilo ndilo eneo rahisi zaidi la timu kutabiri kwamba linaweza kufikia kiwango cha juu msimu ujao, lakini bado kuna maswali makubwa upande mwingine.

Takwimu binafsi za Antetokounmpo katika mashambulizi ni za kushangaza.

Kabla ya kujaribu kucheza licha ya majeraha kwa sehemu kubwa ya msimu uliopita, alikuwa na misimu mitatu mfululizo akiwa na Bucks ambapo alifunga wastani wa angalau pointi 30 na asisti tano kwa mchezo, yote hayo huku akitupia zaidi ya asilimia 55 kutoka uwanjani. Kwa mujibu wa Stathead, alikuwa nyota wa kwanza kufanya hivyo tangu Kareem Abdul-Jabbar (1972-73) na mmoja kati ya wachezaji watatu pekee katika historia ya NBA kufanya hivyo.

Kuelekea mchezo wa 13 wa msimu uliopita, ule ambao alipata jeraha lake kubwa la kwanza, Antetokounmpo alikuwa akifunga wastani wa pointi 32.6, ribaundi 11.3 na pasi za mwisho 7.1 kwa mchezo huku akitupia mitupo bora kwa asilimia 63.

Ili kuweka wazi, Antetokounmpo hakusanyi tu takwimu nyingi kwa ajili yake mwenyewe. Bucks haikuwahi kuwa na kiwango cha mashambulizi kushuka chini ya asilimia 83 katika ligi wakati Antetokounmpo akiwa uwanjani katika misimu minane iliyopita, na kiwango cha mashambulizi wakiwa naye uwanjani kilikuwa zaidi ya asilimia 90 katika misimu mitatu kati ya minane, kwa mujibu wa Cleaning the Glass.

Baada ya kuwa sehemu ya kikosi kilichokuwa na ufanisi mkubwa zaidi wa mashambulizi katika NBA, msimu wa 2022-23 Antetokounmpo alikuwa sehemu ya angalau kikosi kilichomaliza ndani ya 11 bora kwa ufanisi wa mashambulizi katika kila moja ya misimu minne iliyopita. Kabla ya msimu uliopita, Bucks ilikuwa ndani ya 10 bora katika misimu sita kati ya saba iliyotangulia.

Lakini, timu ilitumia kila kipindi cha mapumziko kuboresha namna ya kujenga timu inayomzunguka Antetokounmpo na kuwatambua wachezaji wanaohitajika ili kuongeza uwezo wa nyota huyo wa All-Star mara 10. Kwa kuwa amekuwa akicheza katika kiwango cha MVP misimu minane iliyopita mambo yalikuwa bora zaidi kwake. Miami kwa kuwa tayari wametumia sehemu kubwa ya rasilimali zao kumnunua Antetokounmpo.

Nafasi tatu zilizobaki kwenye kikosi hicho ni lazima watafute wachezaji wanaoweza kumsaidia staa huyo kutumia fursa inayotokana na mvuto wake kwa walinzi wa wapinzani.


MITUPO YA ALAMA TATU

Katika kujaribu kujenga kikosi cha kushindania ubingwa kinachomzunguka Antetokounmpo, Bucks daima ilijaribu kujaza kikosi chake kwa watupiaji wa mitupo ya alama tatu. Baada ya kumaliza msimu wa 2024-25 ikiwa ya kwanza kwa asilimia ya utupaji wa mipira hiyo, Bucks ilishika nafasi ya pili msimu uliopita na kumaliza ndani ya 10 bora kwa asilimia ya mipira hiyo katika misimu minne kati ya mitano ya mwisho ya Antetokounmpo kikosini.

Ingawa Heat inaweza kutafuta aina tofauti za wachezaji, na kocha mkuu Erik Spoelstra anaweza kuwataka wachezaji kufanya zaidi, itakuwa jambo la maana kutarajia kwamba watatafuta wenye uwezo zaidi wa kurusha mipira ya alama tatu ili kumsaidia nyota huyo.

Msimu uliopita, hakuna mchezaji wa Heat aliyerusha mipira ya alama tatu mingi kwa mchezo kuliko Tyler Herro (majaribio 6.7, asilimia 37.8) na Norman Powell (majaribio 7.1, asilimia 38). Hakuna kati ya wachezaji hao wawili atakayekuwa na Heat msimu huu ujao. Bam Adebayo alitupia  iliyofuata kwa wingi, lakini alifanikiwa kwa asilimia 31.8 tu kati ya mipira 5.1 ya alama tatu aliyojaribu kwa mchezo.

Baada ya Adebayo, Heat ina wachezaji watano kutoka msimu uliopita waliorusha angalau mipira miwili ya alama tatu kwa mchezo ambao ni  Andrew Wiggins (majaribio 4.9, asilimia 41.4), Simone Fontecchio (majaribio 4.7, asilimia 37.5), Nikola Jovic (majaribio 3.6, asilimia 26.9), Davion Mitchell (majaribio 3.3, asilimia 39.5) na Pelle Larsson (majaribio 2.7, asilimia 32.3).

Pia walimuongeza Bobby Portis (majaribio 4.4, asilimia 45.6) katika biashara ya kumnunua Antetokounmpo na kumsaini Tim Hardaway Jr (majaribio 6.9, asilimia 40.7) kama mchezaji huru. Wachezaji wote wawili wangekuwa miongoni mwa wachezaji watatu bora wa Heat kwa mipira ya alama tatu msimu uliopita, lakini bado itahitaji maendeleo kutoka ndani ya timu ili kuo ngeza nafasi inayomzunguka nyota huyo. Pamoja na Antetokounmpo, nafasi za kurusha mipira ya alama tatu huenda zikawa wazi zaidi na zisizokuwa ngumu, lakini wachezaji wenzake watalazimika kuongeza idadi ya mipira wanayorusha au asilimia ili kutoa nafasi kubwa zaidi iwezekanavyo.


KUAMUA NAMNA YA KUJILINDA

Kama ilivyo kwa Antetokounmpo upande wa mashambulizi, uwepo wa Adebayo uwanjani umekuwa ukimaanisha mambo mazuri kwa Heat eneo la ulinzi. Katika misimu mitano iliyopita, vikosi vya Heat vilivyokuwa na Adebayo havijawahi kumaliza chini ya asilimia 75 katika ligi nzima, kwa mujibu wa Cleaning the Glass. Vikosi hivyo vilimaliza msimu wa 2023-24 katika asilimia 89 na ule wa 2021-22 asilimia 94. Msimu uliopita ulikuwa wa kwanza kwa Heat kumaliza nje ya 10 bora kwa kiwango cha ulinzi tangu msimu wa 2014-15.

Juhudi za Antetokounmpo katika ulinzi zimepungua kwa miaka ya karibuni kutokana na kuongezeka kwa majukumu ya mashambulizi, lakini uwezo wake wa kujilinda hauna shaka. Ana kasi, nguvu na akili ya kuwalinda wachezaji wa nafasi mbalimbali na kuwa na athari kubwa. Wiggins ana uwezo mzuri na anaweza kuwalinda vyema mawinga huku pia akiwa mlinzi mwenye akili katika timu. Mitchell ni mmoja wa walinzi wanaokera zaidi NBA dhidi ya ‘point guards’.

K wa wachezaji hao wanne, Heat ina msingi wa kundi ambalo linapaswa kumaliza msimu ndani ya 10 bora, ikiwa siyo tano bora, kwa kiwango cha ulinzi. Ili ipate kiwango cha juu kutoka kwa wachezaji wake wenye vipaji zaidi vya ulinzi, kocha atalazimika kuamua hasa namna ya kuwatumia.

Katika misimu mitano iliyopita, msingi katika ulinzi umekuwa kiwango cha chini cha ‘free throw’, uwezo mkubwa wa kuchukua ribaundi za ulinzi na kupunguza mipira inayoruhusiwa kufika kwenye kikapu. Kwa kutowapeleka timu pinzani kwenye mstari wa ‘free throw’ mara nyingi, kupunguza nafasi za pili za kufunga na kutoruhusu timu kufika hadi kwenye kikapu, Heat imepunguza fursa za wapinzani kupata pointi rahisi zaidi.

Imefanya yote hayo huku pia ikiwa miongoni mwa timu zenye uchezaji wa nguvu zaidi NBA na kutumia mifumo ya ulinzi yenye mchanganyiko mpana zaidi kuliko karibu timu yoyote kwenye ligi hiyo.

Kwa mujibu wa takwimu, Heat ilibadilisha walinzi katika asilimia 38 ya ‘pick-and-roll’ walizolinda msimu uliopita, ambayo ilikuwa nafasi ya tatu nyuma ya Brooklyn Nets na Los Angeles Lakers. Zaidi ya hapo, Heat ilikuwa ndani ya tano bora kubadilisha walinzi misimu ya 2021-22 na 2022-23.

Spoelstra pia amekuwa mmoja wa makocha wanaotumia zaidi mikakati ya ‘zone defence’ kwenye ligi. Mwisho wa yote, Heat ina walinzi wenye vipaji, na wanafundishwa na mmoja wa watu wenye ubunifu mkubwa zaidi katika ulinzi kwenye NBA. Uwezekano mkubwa ni kwamba watakuwa miongoni mwa timu bora za ulinzi msimu ujao; suala ni namna Spoelstra atakavyowatumia wachezaji wake kufanikisha hilo.