Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haya Gyokeres kaelewa somo

GYOKERES Pict (1)

Muktasari:

  • Staa huyo wa Sweden ameamua kubadili mpango wake kwenye usajili huo, akifuta kipaumbele cha kwenda Arsenal na kufungua milango upya ya kwenda kucheza chini ya Kocha Ruben Amorim huko Old Trafford ili kuirudisha timu hiyo kwenye makali yake ya kushindania mataji.

LISBON, URENO: STRAIKA, Viktor Gyokeres ameiweka Manchester United kwenye klabu namba moja inayoweza kunasa saini yake dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Staa huyo wa Sweden ameamua kubadili mpango wake kwenye usajili huo, akifuta kipaumbele cha kwenda Arsenal na kufungua milango upya ya kwenda kucheza chini ya Kocha Ruben Amorim huko Old Trafford ili kuirudisha timu hiyo kwenye makali yake ya kushindania mataji.

Gyokeres, 27, amekuwa akisakwa na timu nyingi kwenye dirisha hili.

Na mwenyewe yupo tayari kuachana na Sporting Lisbon, mahali ambako amefunga mabao 54 katika mechi 52 msimu uliopita.

Gyokeres anataka kujaribu upya kiwango chake kwenye ligi kubwa wa Ulaya, lakini hadi sasa hakuna timu iliyoweka mezani ofa rasmi ya kunasa huduma ya mkali huyo.

Sporting ilisisitiza kwamba haijapokea ofa kuhusu mchezaji huyo, huku rais wa klabu hiyo, Frederico Varandas ameshutumiwa kumdanganya mchezaji huyo kuhusu dili linaloweza kumng’oa staa huyo kuwa ni Pauni 59 milioni.

Kambi ya mawakala wa Gyokeres inadai Sporting inataka pesa nyingi sana kwenye mauzo ya mchezaji huyo, ikitaka Pauni 86 milioni - kwa mchezaji ambaye amefunga mabao 97 katika mechi 102  tangu alipotua Ureno akitokea Coventry City miaka miwili iliyopita.

Kumeelezwa kuna malumbano baina ya pande hizo mbili, ikidaiwa Gyokeres hatarudi kwenye kikosi hicho kwa ajili ya pre-season. Straika huyo aligomea uhamisho wa kwenda Saudi Arabia mwezi uliopita. Al-Hilal ilipeleka ofa ya Pauni 55 milioni, lakini ilikataliwa na Sporting, huku Gyokeres akiweka wazi hana mpango wa kuhamia Mashariki ya Kati, anataka aendelee zake kutamba kwenye soka la Ulaya.

Real Madrid imesema haina mpango wa kumsajili, wakala Liverpool imefuta mpango huo. Alihusishwa na Juventus, lakini haina pesa ya kutosha kunasa saini yake na Bayern Munich inaye Harry Kane, wakati Paris Saint-Germain kocha Luis Enrique hamhitaji kama ilivyo kwa Barcelona.

Hilo lilifanya Arsenal na Man United kubaki zenyewe kwenye vita ya kumtaka straika huyo, kutokana na timu hizo mbili zote kuhitaji mtu mpya kwenye eneo hilo.

Lakini, mkurugenzi wa michezo mpya wa Arsenal, Andrea Berta mipango yake ipo kwa straika wa RB Leipzig, Benjamin Sesko kwa sababu anapatikana kwa gharama nafuu na umri wake ni mdogo.

Kutokana na hilo, Gyokeres sasa anafikiria kwenda Man United kuungana na kocha wake wa zamani, Amorim kwenda kuanzisha zama mpya kwenye timu licha ya kwamba haitakuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.