Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Harry Kane anahesabu siku tu kwa sasa

Muktasari:

  • Kane anayepambana kusaka taji la kwanza la Ligi tangu aanze kucheza soka kuanzia England, anasikilizia mechi hizo kati ya sita zilizosalia kufungia msimu ili kubeba ubingwa na Bayern na kuandikia rekodi binafsi baada ya msimu uliopita kutoka kapa.

HARRY Kane, jana usiku alifunga bao moja wakati Bayern Munich ikipata ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Augsburg katika Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga huku nyota huyo wa Uingereza akibakiwa na mechi nne tu kuandika rekodi binafsi.

Kane anayepambana kusaka taji la kwanza la Ligi tangu aanze kucheza soka kuanzia England, anasikilizia mechi hizo kati ya sita zilizosalia kufungia msimu ili kubeba ubingwa na Bayern na kuandikia rekodi binafsi baada ya msimu uliopita kutoka kapa.

 Mshambuliaji na nahodha huyo wa timu ya taifa ya England, alifunga bao la 23 kwake msimu huu na lililokuwa la pili kwa mchezo wa jana dakika ya 60 alimalizia pasi ya Michael Olise ikiwa ni dakika moja baada ya Augsburg kupata pigo kwa Cedric Zesiger kuonyeshwa kadi ya pili ya njano iliyozaa nyekundu kutokana na kucheza madhambi.

Mabao mengine katika mchezo huo yaliwekwa kimiani na Jamal Musiala dakika ya 42 ikiwa ni la kusawazisha baada ya wenyeji kutangulia kwa bao la Dimitrios Giannoulis dakika ya 30.

 Hata hivyo, Musiala hakumaliza mchezo kwani aliumia kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Thomas Muller dakika 54. Bao la tatu la Bayern lilifungwa dakika za nyongeza baada ya Chrislain Matsima kujifunga katika harakati za kuokoa mpira sekunde chache kabla ya Kane na Leroy Sane kupumzishwa katika mchezo huo.

Ushindi huo umeifanya The Bavarians kufikisha pointi 68 kutokana na mechi 28 na kukata tiketi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa klabu ya kwanza kutoka Bundesliga, pia ikihitaji pointi 13 tu katika mechi sita zilizobaki ili itawazwe bingwa Ligi hiyo.

Kama Bayern ikivuna pointi hizo 13 itafikisha 81 ambazo hazifikiwa na timu yoyote ikiwamo watetezi Bayer Leverkusen iliyopo nafasi ya pili kwa sasa ikiwa na pointi 59 kupitia michezo 27 na ikiswaliwa na mechi saba ambazo ikishinda zote itafikisha 80 tu.

Ushindi wa jana kwa Bayern ulikuwa ni wa 21 msimu huu, ikifikisha pia mabao 81 na kufungwa 27, ikiwa na uwiano wa 54 hadi sasa kulinganisha na 28 na Leverkusen inayotarajiwa kushuka uwanjani jioni ya leo ikiwa ugenini dhidi ya Heidenheim.

Mechi sita zijazo za kufungia msimu kwa Bayern, huku ikihitaji nne za kwanza kushinda zote ili kubeba taji la 34 la Bundesliga ni dhidi ya Borussia Dortmund, Heidenheim, Mainz, RB Leipzig Borussia Monchengladbach na Hoffenheim.