Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres bado mtihani, vigogo wajaa vitani

VITA Pict

Muktasari:

  • Rais wa Sporting, Frederico Varandas alijibu ripoti kwamba Gyokeres alikuwa ‘amekasirika’ na kugoma baada ya timu kushindwa kuheshimu makubaliano waliyowekeana na mchezaji huyo mwanzoni mwa mwezi huu ambayo ilikuwa ni kumruhusu kuondoka kwa Euro 80 milioni badala ya Euro 100 milioni ambazo zipo katika mkataba.

LONDON, ENGLAND: LICHA ya ripoti kwamba uhusiano baina ya straika Viktor Gyokeres na uongozi wa klabu yake ya Sporting Lisbon kutokuwa mzuri hivi karibuni, bado vigogo mbalimbali wakiwamo Arsenal na Manchester United wameendelea kufanya mazungumzo na wawakilishi wa staa huyo ili kumsajili katika dirisha lijalo.

Rais wa Sporting, Frederico Varandas alijibu ripoti kwamba Gyokeres alikuwa ‘amekasirika’ na kugoma baada ya timu kushindwa kuheshimu makubaliano waliyowekeana na mchezaji huyo mwanzoni mwa mwezi huu ambayo ilikuwa ni kumruhusu kuondoka kwa Euro 80 milioni badala ya Euro 100 milioni ambazo zipo katika mkataba.

Varandas alidai kuwa ‘vitisho, ulazimishaji na matusi’ havitamsukuma abadili msimamo wake na kusisitiza kwamba hakuwahi kumuahidi mchezaji huyo au wakala wake kuwa ataondoka kwa ada ya bei ya chini.

Kauli za rais huyo zinadaiwa kutikisa soko la usajili kwani timu nyingi ziliamiani zingempata kwa kiasi kilichokuwa kinatajwa zamani.

Hata hivyo, mazungumzo baina ya wakala wa Gyokeres na wawakilishi wa timu hiyo bado yanaendelea na inadaiwa wakala wake yuko London tayari.

Arsenal iko sokoni ikisaka mshambuliaji na mbali ya Gyokeres pia imehusishwa na usajili wa mshambuliaji wa RB Leipzig, Benjamin Sesko, ambaye ndio kipaumbele kwa sasa.

Wiki iliyopita, Arsenal iliripotiwa kuwasilisha ombi rasmi kwa Leipzig kujua bei halisi ya Sesko.

Inaripotiwa kuwa Leipzig inataka kumuuza Sesko kwa pesa ndefu sawa na zile zinazotajwa kwa Alexander Isak  wa Newcastle na mastaa wengine wanaosumbua sokoni, lakini Arsenal inaamini inaweza kumpata kwa Pauni 70 milioni.

Arsenal pia ina matumaini ya kumpata Gyokeres kwa ada ileile inayotajwa kuwa ni makubaliano ya mchezaji na timu hapo awali, lakini rais wa Sporting Varandas alihakikishia kuwa Gyokeres hataondoka kwa bei hiyo.

“Mchezo huu unaochezwa na wakala unazidisha hali kuwa mbaya zaidi. Hadi leo, Sporting haijapokea ofa yoyote kwa Viktor Gyokeres, si leo wala msimu uliopita.”

Rais huyo alikiri kuwa kulikuwa na makubaliano kuhusu ada iliyopo katika kifungu cha kumwachia mchezaji kutotolewa chote, lakini hawakusema kwamba ni kiasi gani kinapaswa kutolewa, tofauti kabisa na inavyoonekana mitandaoni.

Katika mkataba wake wa sasa staa huyu amebakisha miaka mitatu lakini hana mpango wa kuendelea kusalia katika  timu hiyo.

Kocha wa Sporting Rui Borges, aliulizwa kuhusu Gyokeres Jumanne iliyopita akasema: “Gyokeres? Mustakabali wa Sporting unaanza Julai 1. Hilo tu ndilo naweza kusema.”