Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gwiji Man United amtolea uvivu Benjamin Sesko

SESKO Pict

Muktasari:

  • Rooney ameeleza mtazamo wake kupitia kipindi chake cha podcast cha Stick to United, ambapo alionyesha kutofurahishwa na kutokuwepo kwa Sesko kwenye kikosi cha United katika mchezo huo wa Jumapili iliyopita.

MANCHESTER, ENGLAND: GWIJI wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, amemkosoa mshambuliaji wa klabu hiyo, Benjamin Sesko, kwa kukosa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Fulham uliomalizika kwa sare ya 1-1, akitilia shaka uzito wa jeraha la mguu lililomfanya Mslovenia huyo asishiriki.

Rooney ameeleza mtazamo wake kupitia kipindi chake cha podcast cha Stick to United, ambapo alionyesha kutofurahishwa na kutokuwepo kwa Sesko kwenye kikosi cha United katika mchezo huo wa Jumapili iliyopita.

“Jeraha la mguu? Amevunjika?” Rooney alihoji. “Unaweza kuumia kwenye mguu, unaweza kukutana na changamoto kwenye mchezo... Nadhani pia amevaa zile kinga ndogo za mguu zinazokera.”

SESK 04

Nahodha huyo wa zamani wa United aliendelea kukosoa uamuzi wa Sesko kutocheza, akisema: “Ikiwa unajaribu kucheza kama namba tisa kwa Manchester United, una mchezo ambao lazima ushinde, halafu una maumivu kwenye mguu na huchezi... hiyo ni sehemu kubwa ya tatizo.”

Rooney pia alikumbuka kipindi chake akiwa mchezaji wa United, akisema wachezaji walitarajiwa kucheza hata wakiwa na majeraha, isipokuwa pale ambapo walikuwa hawawezi kabisa kuendelea.

“Isipokuwa kama huwezi kabisa kucheza, unacheza ukiwa umeumia. Nakumbuka kabla ya mechi tulikuwa tunapatiwa sindano, na daktari alikuwa akizichoma kwenye makalio,” amesema.


SESK 01

SCHOLES, BUTT NAO WAMO

Wachezaji wengine wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes na Nicky Butt, pia walieleza wasiwasi wao kuhusu kutokuwepo kwa Sesko katika kikosi kilichocheza dhidi ya Fulham.

Katika podcast yao, The Good, The Bad & The Football with Paddy McGuinness, Scholes aliunga mkono mtazamo wa Rooney.

“Ikiwa hajavunjika, basi avae kinga zake za mguu,” Scholes amesema.

Butt naye akaongeza: “Wewe ni mchezaji, ama umevunjika mguu au huchezi!”

Kauli hizo hazikupokelewa vizuri nchini Slovenia. Kama ilivyoripotiwa na Daily Mail Sport, beki wa Leeds United na timu ya taifa ya Slovenia, Jaka Bijol, alimtetea Sesko na kumtaka asikubali presha hiyo imwathiri.

“Natumaini na naamini kwamba Beni anajua jinsi ya kujitenga na aina hii ya presha,” Bijol amesema.

SESK 06

“Wakati mambo hayaendi vizuri uwanjani na una mashaka fulani, kusoma kauli kama hizi kunaweza kufanya hali ya kujiamini kuwa mbaya zaidi.

“Hapaswi kuzizingatia sana, kwa sababu sote tunajua ana ubora gani. Yeye mwenyewe anajua ni mchezaji wa aina gani, na nadhani huwa anaonyesha hilo kila mara kupitia mambo ya kipekee anayofanya uwanjani.”

Mshambuliaji mwingine wa Slovenia, Zan Vipotnik wa Swansea City, pia alimtetea Sesko, akisema hali anayopitia si rahisi.

SESK 05

“Si rahisi kwake. Matatizo ya mara kwa mara ya kimwili ni mabaya, na zaidi ya hayo yanaweza kuathiri akili yako,” Vipotnik amesema.

“Natumaini na naamini kwamba kutokuwepo kwake uwanjani kutakuwa kwa muda mfupi iwezekanavyo na kwamba mambo yatabadilika kuwa mazuri hivi karibuni.”