Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Grealish anaondoka Man City na kibunda chake

GREALISH Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, nyota huyo ambaye alisajiliwa akitokea Aston Villa mwaka 2021, hataondoka kinyonge kwani ni mmoja wa wachezaji waliokuwa wanalipwa pesa nyingi katika Ligi Kuu England na huenda akaendelea kulipwa mshahara mnono huko atakakokwenda na kuendelea kusihi kibosi.

MANCHESTER, ENGLAND: KUNA stori zinasambaa huenda nyota wa Manchester City, Jack Grealish akapewa mkono wa kwaheri na miamba hiyo baada ya kudumu kwa takriban miaka minne.

Hata hivyo, nyota huyo ambaye alisajiliwa akitokea Aston Villa mwaka 2021, hataondoka kinyonge kwani ni mmoja wa wachezaji waliokuwa wanalipwa pesa nyingi katika Ligi Kuu England na huenda akaendelea kulipwa mshahara mnono huko atakakokwenda na kuendelea kusihi kibosi.

Inawezekana pia asiende timu itakayomlipa pesa ndefu kama ilivyokuwa kwa Man City, lakini nyota huyo kwa utajiri alionao hatatetereka kutokana pia na kuwa na madili mengine nje ya soka yanayomfanya azidi kuwa tajiri. Hata hivyo, unajua utajiri wake upoje?

GRE 01

ANAVYOPIGA PESA

Alipojiunga na Man City akitokea Aston Villa kwa kitita cha Paui 100 milioni mwaka 2021, Grealish alisaini mkataba unaomlipa mshahara wa takribani Pauni 300,000 kwa wiki.

Kiasi hicho kimemweka katika orodha ya wachezaji wanaolipwa vizuri zaidi katika Ligi Kuu England na kwa msimu mmoja anapata Pauni 15 milioni.

Mbali ya mshahara wake mnono, pia anapata pesa kutokana na kuwa balozi wa kampuni mbalimbali kubwa ikiwamo Puma aliyosaini nayo mkataba mwaka 2023 baada ya kuachana na Nike na una thamani ya pauni 10 milioni.

Pia ni balozi wa kampuni ya Gucci, Bose, EA Sports, Red Bull, McDonald’s na kwa jumla anapata zaidi ya Pauni 7 milioni kwa mwaka na inakadiriwa ana utajiri unaofikia Dola 60 milioni.

GRE 04

NYUMBA

Grealish anaishi katika jumba la kifahari mjini Manchester linalokadiriwa kuwa na thamani ya Pauni 5 milioni, likiwa na chumba cha mazoezi, ukumbi wa sinema binafsi, bwawa la kuogelea, chumba cha michezo ya video.

Pia anamiliki nyumba nyingine maeneo ya Midlands karibu na Birmingham.

GRE 05

MSAADA KWA JAMII

Licha ya maisha yake ya kifahari na utukutu wake, Grealish ni mtu mwenye moyo wa kutoa na amekuwa akitoa misaada katika hospitali na taasisi za watoto na ni mdau wa kudumu wa hospitali ya watoto ya Birmingham na mara kadhaa ameonekana katika vituo vya watoto yatima huko Birmingham akitota misaada.

Taasisi nyingine za kijamii ambazo amewahi kuzisaidia kwa kufanya kampeni ya kuchangisha na kutoa pesa zake mwenyewe ni pamoja na Young Epilepsy, Special Olympics GB, Mind (Mental Health Charity) na Make-A-Wish Foundation UK.

GRE 02

MAISHA NA BATA

Grealish anapenda burudani, mara nyingi huonekana maeneo ya starehe kama  Ibiza, Mykonos, Dubai na Las Vegas akiwa na marafiki au wachezaji wenzake.

Kwa sasa yupo kwenye mahusiano na Sasha Attwood ambaye ni mpenzi wake wa muda mrefu.