Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Giza ishu ya Christian Eriksen kustaafu

ERIKSEN Pict

Muktasari:

  • Eriksen, ambaye aliwahi kuzichezea Manchester United na Tottenham Hotspur, aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupata matatizo ya moyo wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya Denmark na Ukraine mwishoni mwa wiki iliyopita.

COPENHAGEN, DENMARK: KIUNGO nyota wa Denmark, Christian Eriksen, amesema hana mpango wa kustaafu soka kwa sasa licha ya kuanguka tena uwanjani katika tukio lililozua hofu kwa mashabiki na wadau wa mchezo huo duniani.

Eriksen, ambaye aliwahi kuzichezea Manchester United na Tottenham Hotspur, aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupata matatizo ya moyo wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya Denmark na Ukraine mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, alianguka ghafla uwanjani baada ya kushika kifuani, lakini kifaa maalumu cha kudhibiti mapigo ya moyo (ICD) alichowekewa baada ya mshtuko wa moyo alioupata 2021 kikifanya kazi ya kurejeshea mapigo ya moyo wake.

ERI 03

Akizungumza kupitia taarifa rasmi, Eriksen amesematukio hilo ni tofauti la 2021 ambalo lilishtua dunia nzima wakati wa michuano ya Euro.

“Kama wengi wanavyoweza kufikiria, kupata mshtuko kutoka kwenye kifaa changu cha ICD kumeathiri sana mimi na familia yangu. Hata hivyo, nataka kuwahakikishia wote kuwa hali hii ni tofauti na ile ya mwaka 2021. Najisikia vizuri na tayari nimeanza safari ya kupona,” amesema Eriksen.

Aliongeza kuwa kwa sasa anajikita katika kuimarisha afya yake, kutumia muda na familia pamoja na kwenda likizo kabla ya kufanya maamuzi yoyote kuhusu mustakabali wake wa soka.

ERI 02

“Ninashukuru sana msaada kutoka kwa wachezaji wenzangu, madaktari na kila aliyekuwa karibu nami. Kifaa changu kilifanya kazi yake kikamilifu na kunilinda wakati nilipohitaji msaada huo. Kwa sasa ninataka kupona, kuwa na familia yangu na kucheza soka na watoto wangu,” amesema.

Hata hivyo, kauli hiyo haijawazuia baadhi ya wadau wa soka kuamini kuwa ni wakati wa Eriksen kutundika daruga.

Aliyekuwa kiungo wa Real Madrid na Everton, Thomas Gravesen, amesema afya na maisha ya Eriksen yanapaswa kupewa kipaumbele kuliko soka.

“Hili si suala la kazi tena, ni suala la maisha ya Christian Eriksen. Tulimwona mke wake akihangaika tena baada ya tukio hili. Lazima afikirie zaidi ya soka. Mchezo huu hauna maana wakati maisha yako yapo hatarini,” amesemaGravesen.

ERI 01
ERI 01

Kwa upande wake, daktari bingwa wa moyo Henning Molgaard, ameeleza kuwa kifaa cha ICD ndicho kilichookoa maisha ya Eriksen, lakini akaonya kuwa hali kama hiyo inaweza kujirudia siku zijazo.

“Kifaa chake kimefanya kazi iliyokusudiwa na bila shaka kimeokoa maisha yake. Matukio kama haya yanaweza kutokea tena kwa watu wenye matatizo ya moyo. Tofauti ni kwamba kwa Eriksen yalitokea akiwa katikati ya uwanja wa mpira,” amesemaMolgaard.

Daktari huyo pia alieleza kuwa klabu vingi vya kitaaluma vinaweza kusita kuendelea kumtumia mchezaji huyo kutokana na hatari ya tukio kama hilo kujirudia.

Daktari wa timu ya taifa ya Denmark, Morten Boesen, aliyesifiwa kwa kuokoa maisha ya Eriksen mwaka 2021, amesemamchezaji huyo alikuwa na fahamu zote mara baada ya tukio hilo na hata alitaka kwenda kuwasalimia familia yake kabla ya kupelekwa hospitalini.

Picha za televisheni zilionyesha Eriksen, akianguka mbali na mpira katikati ya kipindi cha pili cha mchezo huo dhidi ya Ukraine. Madaktari waliingia haraka uwanjani kumpatia huduma za dharura huku mchezo ukisitishwa mara moja.

Shirikisho la Soka la Denmark lilithibitisha baadaye kuwa Eriksen alikuwa katika hali nzuri kulingana na mazingira ya tukio hilo, huku mashabiki waliokuwapo uwanjani wakianza kuimba jina lake na kumpigia makofi kama ishara ya kumuombea nafuu.

Tukio hilo liliwaacha wachezaji wengi wa Denmark wakiwa na huzuni kubwa, baadhi yao wakishindwa kuzuia machozi, huku aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Nicklas Bendtner, akieleza kushtushwa na tukio hilo.

“Haya ni matukio ya kuumiza sana. Mawazo yangu yako kwa familia yake na watoto wake. Hii ni mara ya pili kutokea kwa Christian, na kama rafiki yake, ni jambo la kusikitisha mno,” amesemaBendtner.

Eriksen kwa sasa ana mwaka mmoja uliobaki katika mkataba wake na klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani, lakini bado haijafahamika iwapo ataendelea kucheza soka la ushindani baada ya kupona.