Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fury: Pambano na Anthony Joshua limekwama!

PAMBANO Pict

Muktasari:

  • Mabondia hao wawili wakubwa kutoka England walionekana kuwa kwenye hatua nzuri ya kukutana mwishoni mwa mwaka huu, lakini Fury amekuwa akimtuhumu mpinzani wake kwa kuchelewesha makubaliano ya kimkataba.

LONDON, ENGLAND: BONDIA wa ngumi za uzito wa juu duniani, Tyson Fury amedai kuwa pambano lake dhidi ya Anthony Joshua (AJ), huenda lisifanyike baada ya kuibuka tena kwa mvutano kuhusu mkataba na eneo litakalotumika kuandaa hilo.

Mabondia hao wawili wakubwa kutoka England walionekana kuwa kwenye hatua nzuri ya kukutana mwishoni mwa mwaka huu, lakini Fury amekuwa akimtuhumu mpinzani wake kwa kuchelewesha makubaliano ya kimkataba.

Promota wa Joshua, Eddie Hearn, wiki iliyopita amesema mazungumzo yalikuwa yamefunguliwa tena, lakini kwa kuaminiwa Fury mambo yameanza kurudi tena nyuma. “Kwa hiyo inaonekana AJ amejisaidia tena kwa hofu. Baada ya miaka 11, hatimaye amejisaidia tena,† Fury amesema kupitia mitandao ya kijamii.

Mvutano mkubwa kuhusu pambano hilo la uzito wa juu umejikita zaidi kwenye eneo litakalopigwa, ambapo upande mmoja unatamani lifanyike kwenye Uwanja wa Wembley, London, wakati watangazaji Netflix wanapendelea Madison Square Garden jijini New York, Marekani.

PAMB 01

Fury, ambaye mara kwa mara hutumia mitandao ya kijamii kutoa maoni yake kuhusu wapinzani wake, wiki iliyopita alisisitiza kuwa haamini kama Joshua ana mapenzi makubwa na nchi yake, ambapo mapema mwaka huu iliripotiwa aliondoka England na kuhamia Dubai.

Fury pia alizungumzia kauli ya Joshua ya mwaka 2020 katika maandamano ya Black Lives Matter, ambapo alisoma barua kutoka kwa rafiki yake Reece Campbell iliyowataka waandamanaji kuacha kutumia fedha katika maduka na biashara zinazomilikiwa na wazungu.

“Waonyeshe sehemu wanayoumia,” amesema  Joshua katika maelezo yake akiwataka watu kuacha kutumia fedha katika biashara hizo na kuwekeza katika zile zinazomilikiwa na watu weusi.

Fury alichapisha tena video ya hotuba hiyo na kuandika ujumbe mkali akimshambulia Joshua, akisema: “Ni huyu mtu anayesema anaipenda England? Mtu asiye na ujasiri kabisa! Mnyanyasaji asiye na maana! Msidanganywe! Na anaishi Dubai.”

PAMB 02

Katika video nyingine, Fury alimtuhumu Joshua kwa kujaribu kuvuruga pambano kwa kuhofia kuaibishwa.

“Hata endapo ningekubali kufungwa mikono yote miwili nyuma ya mgongo na kuvaa viatu vya saruji, Anthony Joshua bado asingethubutu kuingia ulingoni na mimi, kwa sababu nitamuangamiza,”  amesema Fury. Pia alimtuhumu kuwa ni mnyanyasaji akidai tabia hiyo ilionekana katika pambano lake dhidi ya Daniel Dubois, ambapo Joshua alipoteza kwa knockout.

Akizungumzia madai kwamba hataki pambano lifanyike England, Fury amesema: “Tyson hataki kupigana England? Kwa nini nisitake kupigana England? Tyson anataka kupigana Marekani? Mnaongea kweli?”

Fury alisisitiza kuwa yeye siyo mtu anayependa fedha kwa ajili ya pambano hilo na kwamba, uamuzi mkubwa uko kwa Netflix na mfanyabiashara wa Saudi Arabia, Turki Al-Sheikh aliye tayari kuwaandalia mechi.

PAMB 03

“Tyson haongozi pambano hili. Tyson hajaweka fedha kwenye pambano hili. Tyson siyo mfadhili mkuu. Netflix na Turki Al-Sheikh ndio wanaohusika,” amesema na kwamba endapo litafanyika England atafurahia zaidi.

“Wembley, saa 10 jioni, watu 100,000. Kwa nini nisitake pambano hilo lifanyike England? Haina maana kusema sitaki.”

Fury alimshambulia zaidi Joshua pamoja na promota wake Eddie Hearn, akisema hakuna mahali AJ atakapoweza kujificha.

PAMB 04

“Nitakuja Watford, nitakupiga kwenye uwanja wako wa nyumbani. Hakuna namna ya kulikwepa pambano hili. Jiandae. Nimechoka na mambo yako kwa miaka 11. Nitakupiga vibaya sana,”€  amesema.

Akiendelea kutumia jina lake la utani ‘Gypsy King’€ , Fury amesema Joshua ataanguka€ na kwamba baada ya pambano hilo hataweza tena kuonekana hadharani, huku akimkejeli kwa uwezo wake wa mwili na kasi akisema ana misuli mingi lakini hana kasi ya kutosha.

Promota wa Fury, Frank Warren, wiki iliyopita alidokeza kwamba makubaliano dhidi ya AJ yalipaswa kukamilishwa Jumapili.

“AJ bado hajasaini. Tyson alisaini Januari. Anaendelea na maandalizi Miami kwa ajili ya pambano la mapema Novemba na hajali litafanyika wapi,” Warren amesema.


PAMB 05

SASA AMGEUKIA USYK

Fury alifichua kuwa ameanza kulenga pambano la tatu dhidi ya Oleksandr Usyk, licha ya kupoteza mawili ya awali dhidi ya bondia huyo wa Ukraine.

“Kwa hiyo jambo hili linanielekeza kwenye pambano dhidi ya Oleksandr Usyk. Tulifanye tena. Turudie Novemba. Mpira sasa uko upande wako, Oleksandr,” amesema na kuongeza:

“Unataka kupigana nami mwaka huu, 2026, au umeamua kustaafu? Nijulishe, kwa sababu sasa natafuta mpinzani mpya.”