Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fury, Joshua wamekuwa vivuli vya walivyokuwa

PAMB 02

LONDON, ENGLAND: “WATAZICHAPA, hawatazichapa?” Hiyo imekuwa kama tamthilia isiyo na mwisho, huku maneno yenye matusi miongoni wao ya hivi karibuni yakiacha ladha chungu kwa mashabiki katika kulitafakari pambano kati ya mabondia hayo wa ngumi za uzito wa juu duniani ambalo limekuwa likipigwa danadana kwa miaka mingi.

Kwa karibu muongo mmoja sasa, Tyson Fury na Anthony Joshua wamekuwa wakizungukana, wakitupiana vijembe na matusi kuhusu madhara watakayosababishiana mara tu makubaliano ya pambano la uzito wa juu la karne ya 21 ambalo limeshapewa jina la  ‘Vita vya Waingereza’

“Uko wapi, kijana? Nakuja kwa ajili yako, mshenzi wewe,” Fury alimdhihaki Joshua mwaka 2017, wakati ambao ni muda mrefu uliopita kiasi kwamba Moses Itauma alikuwa bado hajaanza hata shule ya sekondari, kabla ya kuja kuwa bondia maarufu na mkubwa huko Ulaya.

Miaka tisa baadaye, hali haijabadilika, huku anayejiita Gypsy King (Fury) akiendelea kuandika kwa hamu kubwa kwenye mitandao ya kijamii akieleza jinsi alivyo na shauku kubwa ya kumuangamiza mpinzani wake anayemuita “mjenga mwili”, kiasi kwamba yupo tayari hata kukubali pambano hilo lifanyike kwenye uwanja wa nyumbani wa Joshua huko Watford, England.


PAMB 05

LINI SASA?

Hata hivyo, kwa kuzingatia kwamba pambano hilo limekuwa likizungumzwa katika mabara matatu na bado halijawahi kutokea, kauli hiyo inaweza kwa mantiki kuchukuliwa kuwa ni majigambo yasiyo na uzito, hasa kwa sababu Joshua kwa sasa anaishi Dubai.

Mchezo huu umejaa chumvi na kutia mambo chumvi kiasi kwamba hata PT Barnum (promota wa zamani sana duniani aliyekuwa maarufu zaidi katika ngumi) huenda angefikiria mara mbili kabla ya kuupigia debe.

Leo, wababe hao wawili wa ndondi za Uingereza wamekuwa vivuli vilivyofifia vya watu waliokuwa zamani; pambano la hivi karibuni la Fury lililofanyika katika ukumbi wa mazoezi nchini Thailand dhidi ya Mpolandi mwenye umri wa miaka 46, Mariusz Wach, lilikuwa la kiwango cha chini kiasi kwamba halikuonyeshwa moja kwa moja na kituo chochote cha televisheni wala jukwaa lolote la mtandaoni, huku Joshua naye akiangushwa mara mbili katika raundi ya kwanza mwezi Julai na Kristian Prenga, Mualbania asiyejulikana sana ambaye anafahamika zaidi kama mpiganaji wa kickboxing.


PAMBANO Pict

NINI KINAFUATA?

Imefikia hatua ambapo walichobakiza mabondia hao wao wenyewe ni kuzichapa tu. Na hata sasa, wakati pambano ambalo zamani lilikuwa likitikisa dunia likifikiriwa upya kama pambano la ana kwa ana kati ya wapiganaji waliopitwa na wakati, kinachosikika ni mapromota wakibishana na mabondia wao wakijifanya na kuonyeshana tambo za kibabe huku wakiaibishana.

Fury, kwa mbali, ndiye mhusika mkuu wa hali hii. Kwa muda mfupi ilionekana kana kwamba alikuwa amegundua utu na busara baada ya ajali mbaya ya gari iliyompata Joshua nchini Nigeria, Desemba iliyopita, ambapo marafiki zake wawili wa karibu walifariki dunia alipomtumia salamu za rambirambi na kusema kwamba janga hilo lilimfanya aamue kurejea ulingoni.

Lakini katika siku za hivi karibuni, huku mabishano zaidi yakiendelea kuhusu iwapo pambano hilo litafanyika kabla au baada ya kipindi kingine, Fury huyo huyo mwenye majigambo na matusi amerejea. Maneno yake ni machungu kuyasikiliza.

“Nitakupiga mpaka kuzimu, wewe mzembe asiye na faida, kipande cha takataka,” Fury alifoka kwenye Instagram, kwa kiwango chake cha kawaida cha ustaarabu. Kwa matusi ya Fury, kama ilivyo katika matangazo yake kuhusu kustaafu, hastahili hata kuheshimiwa kwa kurudiwa, lakini yanasaidia kuchora picha ya mchezo mzima unavyoweza kuwa na mvuto.

“Nitapigana hata Mars,” alijigamba. Katika kambi ya Joshua, Eddie Hearn anasisitiza kwamba mkataba umeshasainiwa, kwamba mazungumzo yanaendelea ili Uwanja wa Wembley uwe mwenyeji badala ya Madison Square Garden ya New York au wakazichape Saudi Arabia.

Hearn anamtuhumu Fury kwa kujaribu kubadilisha masharti na eneo la pambano, Fury naye anamuita “kikaragosi wa kusikitisha” Yaani ni kama tamthilia ya televisheni.

Mbinu ya hivi karibuni ya Fury katika majadiliano ni kudai kwamba pambano hilo limefutwa. Badala yake, anamuita Oleksandr Usyk, mpinzani ambaye amemshinda mara mbili na ambaye anapaswa kupokea ombi akimtaka ulingoni. Katika kipindi cha kusubiri kisicho na mvuto, njia ya uhakika zaidi kwa Fury ya kubaki akizungumziwa ni kuendelea kumchokoza Joshua kwa matusi anayoyatoa.

Fury ana hulka ya kujipendekeza kwa watu wa kiwango cha chini. Ingawa aliwakera baadhi ya mashabiki kwa kujihusisha na vuguvugu la BLM, ambalo lilieleza malengo kama vile kupunguza au kuondoa ufadhili wa polisi, video yake imeondolewa ili kujenga taswira ya jambo ambalo hakulisema. Na Fury, akiwa na hulka ya kujipendekeza anaendelea kulikuza. Unapofikiri amemaliza kabisa akiba yake ya uchokozi wa kijinga, anapata mwingine.


PAMB 01

UWANJA WA CARDIFF

Uwanja wa Principality wa Cardiff umeibuka kuwa chaguo linalopewa nafasi kubwa zaidi kuandaa pambano linalosubiriwa kwa hamu kati ya mabondia Joshua na Fury, huku uwezekano ukionekana pambano hilo kupigwa usiku wa manane au mapema alfajiri.

Mamlaka za eneo hilo zinatarajiwa leo kuamua kuhusu ombi la kuondoa zuio la uwanja huo kufungwa ifikapo saa 4:30 usiku, hatua ambayo inaweza kufungua njia ya pambano hilo kufanyika Cardiff baada ya mvutano kuhusu uwezekano wa kuandaliwa Wembley Stadium, London, au Madison Square Garden, New York.

 Cardiff tayari ina historia ya kuandaa mapambano makubwa ya ndondi nyakati za usiku. Mwaka 2007, bondia Joe Calzaghe alipambana na Mikkel Kessler katika Principality Stadium, huku pambano hilo likianza majira ya saa 8:00 usiku.

Joshua na Fury wanaweza pia kupanda ulingoni muda kama huo ili kukidhi mahitaji ya watazamaji wengi wa televisheni nchini Marekani, ambako pambano hilo linatarajiwa kuonyeshwa na mtandao wa Netflix.