Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nairobi kuandaa mbio za Dunia 2029, yazibwaga London, Rome

RIADHA Pict

Muktasari:

  • Nairobi imeibuka mshindi katika mchakato wa tenda uliohusisha pia majiji ya London (England) na Rome (talia)

Jiji la Nairobi limeandika historia mpya katika riadha duniani baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Dunia ya Riadha ya mwaka 2029 na hivyo kuzima ndoto ya London (England) ya kuandaa mashindano hayo kwa mara nyingine.

Uamuzi huo uliotangazwa leo Jumanne, Septemba 15, 2026 na Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani, Sebastian Coe, umeifanya Kenya kuwa sehemu ya historia ya mashindano hayo, huku Afrika ikipata nafasi ya kwanza kabisa kuandaa tukio hilo kubwa zaidi katika kalenda ya riadha duniani.

Nairobi iliibuka mshindi katika mchakato wa tenda uliohusisha pia majiji ya London (England) na Rome (Rome).

Kwa London, uamuzi huo umekuwa pigo kubwa baada ya jiji hilo kuwasilisha kile kilichoelezwa kuwa “pendekezo lenye mvuto mkubwa”, huku ukipata pia uungwaji mkono wa Serikali ya Uingereza.

Serikali ya England ilikuwa imeahidi takribani Pauni 35 milioni (Sh100 bilioni) kusaidia zabuni hiyo, ikiamini kuwa mashindano hayo yangeongeza shughuli za kiuchumi na kuimarisha zaidi hadhi ya Uingereza kama mwenyeji wa matukio makubwa ya michezo.

RIAD 01

London tayari ina historia nzuri ya kuandaa mashindano hayo. Mji huo uliandaa Mashindano ya Dunia ya Riadha mwaka 2017, ambapo tukio hilo lilipokea mwitikio mkubwa, baada ya viwanja kufurika watu.

Lakini safari hii, Shirikisho la Riadha la Kimataifa, limeamua kupeleka mashindano hayo upande mwingine wa dunia.

Uchaguzi wa Nairobi una umuhimu wa kipekee kwa Afrika, kwani itakuwa mara ya kwanza Mashindano ya Dunia ya Riadha kufanyika katika bara hili.

Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza hadhi ya Kenya na Afrika kwa ujumla katika medani ya michezo ya kimataifa, huku Nairobi ikipata fursa ya kuonyesha uwezo wake wa kuandaa moja ya hafla kubwa zaidi za michezo duniani.

RIAD 02

Kwa nchi kama Kenya, ambayo imejenga jina kubwa kimataifa kupitia mafanikio ya wanariadha wake katika mbio za masafa marefu na ya kati, uamuzi huo unaongeza uzito zaidi kwenye nafasi yake katika riadha duniani.

Wakati Nairobi ikipata nafasi ya kuandaa mashindano ya 2029, jiji la Munich nchini Ujerumani, limepewa haki ya kuwa mwenyeji wa toleo la mwaka 2031.

Uamuzi huo unamaanisha kuwa mashindano hayo yatarudi Ulaya baada ya miaka nane.

London na Rome ndiyo yalikosa nafasi baada ya kushiriki katika mchakato rasmi wa kuwania zabuni hiyo.

Kushindwa kwa London pia ni pigo kwa baadhi ya wanariadha maarufu wa England  ambao walitarajia kushindana mbele ya mashabiki wao katika mashindano ya mwaka 2029.

Miongoni mwao ni Keely Hodgkinson, bingwa wa Olimpiki wa mbio za mita 800, pamoja na wanariadha wengine nyota kama Josh Kerr, Amy Hunt na Georgia Hunter Bell.

RIAD 03

Kwao, mashindano hayo yangekuwa fursa ya kuwania medali mbele ya mashabiki wa nyumbani, lakini sasa ndoto hiyo imefutika.

Uamuzi huo ulitangazwa na Coe kupitia mkutano wa waandishi wa habari uambao umefanyika mapema leo Jumanne, baada ya kumalizika kwa kikao cha siku mbili cha Baraza la Kimataifa la Riadha.

Kwa Nairobi, hata hivyo, huu ni ushindi unaobeba zaidi ya kuandaa mashindano. Ni hatua inayoiweka Afrika katikati ya jukwaa kubwa la riadha duniani na kuifanya Kenya kuingia katika historia kama nchi ya kwanza barani humo kuandaa Mashindano ya Dunia ya Riadha.