Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fukushima: Japan tunalitaka taji

Muktasari:

  • Mwaka 2018 Japan ilibeba taji hilo baada ya kuitandika Hispania mabao 3-1 kwenye fainali iliyopigwa Grenada, Ufaransa.

KIUNGO wa Japan, Noa Fukushima amesema lengo la timu hiyo ni kuhakikisha inarejesha taji la ubingwa walioupoteza mwaka 2018.

Mwaka 2018 Japan ilibeba taji hilo baada ya kuitandika Hispania mabao 3-1 kwenye fainali iliyopigwa Grenada, Ufaransa.

Japan, maarufu kama Young Nadeshiko, inaingia kwenye michuano hiyo ikiwa na matumaini makubwa baada ya kutwaa ubingwa wa Asia wa U-20 mwaka huu nchini Thailand.

Fukushima ni miongoni mwa wachezaji wanaotegemewa kuibeba Japan kutokana na uwezo wake wa kutengeneza nafasi, kushambulia na pia kuwa tishio katika mipira iliyokufa.

Mchezaji huyo tayari ana uzoefu wa mashindano makubwa baada ya kushiriki Kombe la Dunia la Wanawake la U-17 mwaka 2024 na 2025, huku akifunga mabao matatu katika toleo la mwaka jana.

Akizungumza kuanza kwa mashindano hayo, Fukushima alisema ana hamu ya kuonyesha uwezo wake kwenye jukwaa kubwa kama Kombe la Dunia ambalo linafuatiliwa na mamia ya mashabiki ulimwenguni.

Fukushima alisisitiza kuwa nguvu kubwa ya Japan ipo katika umoja wa kikosi, akieleza kuwa hawajengi timu inayomtegemea mchezaji mmoja, bali kila mmoja anajua wajibu wake ndani ya uwanja.

Aliongeza hata wachezaji wanaoanzia benchi ni sehemu muhimu ya mafanikio ya timu hiyo kwa sababu wanaendelea kutoa nguvu na hamasa kwa wenzao hadi filimbi ya mwisho.

Japan pia inaingia Poland ikiwa na kujiamini baada ya kuwafunga Korea Kaskazini katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Asia U-20, matokeo ambayo Fukushima anaamini yamewapa nguvu ya kuamini kuwa wanaweza kushindana na timu yoyote.

“Nataka kushinda wachezaji wa timu zilizopita wamethibitisha kuwa Japan inaweza kushindana na timu yoyote. Tunataka kuonyesha hilo zaidi kwenye Kombe la Dunia na nitatoa kila kitu ili tushinde,” alisema Fukushima.