Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FIFA yamtega Cristiano Ronaldo akikwepa kifungo

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Ronaldo, mwenye umri wa miaka 40, alitolewa nje kwa kumpiga kiwiko Dara O'Shea mgongoni wakati wa mechi ya kufuzu ambapo Ureno ilifungwa 2-0, mapema mwezi huu Novemba 2025.

LONDON, ENGLAND:: Cristiano Ronaldo ataruhusiwa kuichezea Ureno katika mechi yao ya kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 licha ya kuonyeshwa kadi nyekundu dhidi ya Jamhuri ya Ireland, lakini amewekewa mtego.

Ronaldo, mwenye umri wa miaka 40, alitolewa nje kwa kumpiga kiwiko Dara O'Shea mgongoni wakati wa mechi ya kufuzu ambapo Ureno ilifungwa 2-0, mapema mwezi huu Novemba 2025.

Kawaida kosa la kutumia nguvu (violent conduct) hupelekea adhabu ya kufungiwa mechi tatu, lakini Ronaldo amepewa adhabu ya mechi moja tu huku mbili nyingine zikiwa zimesitishwa kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa BBC Sport, ukweli kwamba hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Ronaldo kupewa kadi nyekundu katika mechi 226 za kimataifa umechukuliwa kama sababu ya kupunguzwa kwa adhabu.

Ronaldo alikosa mechi dhidi ya Armenia iliyochezwa Novemba 16, 2025, hivyo hatokosa mechi yoyote nchini Marekani katika Kombe la Dunia 2026 endapo atakuwa fiti.

Taarifa ya FIFA imesema: "Iwapo Cristiano Ronaldo atafanya kosa lingine la aina na uzito kama huo ndani ya kipindi cha majaribio, basi adhabu iliyositishwa itatekelezwa mara moja na atalazimika kutumikia mechi hizo mbili zilizobaki."

Ronaldo amefunga mabao matano katika hatua ya kufuzu huku Ureno ikimaliza kinara Kundi F na kufuzu Kombe la Dunia 2026 kwa mara ya saba mfululizo.

Timu 48 zitajua makundi yao baada ya droo rasmi ambayo itaonyeshwa moja kwa moja na BBC Ijumaa, Desemba 5, 2025.