Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fenerbahce mguu sawa kumnasa Ederson

TETESI Pict

Muktasari:

  • Usajili wa Ederson kwenda Fenerbahce ulifungua njia kwa Gianluig Donnarumma kutua Man City kwani kilichokuwa kinakwamisha ni hicho.

FENERBAHCE wako kwenye hatua za mwisho za kumsajili kipa wa Manchester City, Ederson, 32, dirisha hili.

Usajili wa Ederson kwenda Fenerbahce ulifungua njia kwa Gianluig Donnarumma kutua Man City kwani kilichokuwa kinakwamisha ni hicho.

Licha ya Man City kutaka kumuuza kwanza Ederson ili kumsajili Donnarumma kabla ya dirisha kufungwa, Fenerbahce haina wasiwasi kwani dirisha lao lipo wazi hadi Septemba 13.

Ederson alikuwa akihusishwa kuondoka Man City tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi ikidaiwa kutaka kupata changamoto mpya sehemu nyingine na mbali ya timu za Uturuki, vigogo wa Saudi Arabia pia walihitaji saini yake.

Msimu uliopita alicheza mechi 40 za michuano yote na akamaliza 13 bila ya kuruhusu bao lolote. Mkataba wake na Man City unamalizika mwakani.

Awali Galatasaray ndiyo ilionekana ya kwanza kutaka kumsajili lakini ilishindikana baada ya kugoma kutoa Euro 10 milioni zilizohitajika na City.


Nicolas Jackson

LICHA ya Nicolas Jackson kugoma kurudi London baada ya Chelsea kuiarifu Bayern Munich imeghairi kumtoa staa huyo kwa mkopo, mabosi wa Bayern wamefikia uamuzi wa kujiondoa katika mchakato wa kumsajili staa huyo. Jackson ambaye kwa sasa yupo Ujerumani akiwa amekataa kurudi London baada ya dili kuyeyuka, aliruhusiwa kuondoka kwa sababu hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza lakini baada ya kuumia kwa Liam Delap, Chelsea imesitisha uamuzi wao huyo.


Yves Bissouma

GALATASARAY ya Uturuki ipo katika mazungumzo na Tottenham kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Mali, Yves Bissouma, 29. Bissouma amekuwa Spurs tangu mwaka 2022 aliposajiliwa akitokea Brighton, lakini amekuwa akipata wakati mgumu kupata namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kwa sasa. Mkataba wa sasa wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.


Victor Lindelof

ASTON Villa wako karibu kumsajili beki wa zamani wa Manchester United, Victor Lindelof, 31, kwa uhamisho wa bure, baada ya kuachwa na Manchester United dirisha hili la majira ya kiangazi. Lindelof aliyeicheza Man United tangu mwaka 2017 alipojiunga nao, alicheza jumla ya mechi 250 za michuano yote. Usajili wake unaweza kufanyika muda wowote hata dirisha litakapofungwa kwa sababu ni mchezaji huru.


Roger Fernandes

AL Ittihad ya Saudi Arabia imewasilisha ofa Braga kwa ajili ya kumsajili winga wa klabu hiyo, Roger Fernandes na timu ya taifa ya vijana ya Ureno kabla ya wiki hii kumalizika. Staa huyu ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, msimu huu amecheza mechi saba za michuano yote na kufunga bao moja.  Ittihad inatamani sana kuipata saini yake kwa ajili ya kuhakikisha iboresha eneo la ushambuliaji kwa msimu huu.


Tyrique George

AS Roma ilijiondoa dakika za mwisho za dirisha la usajili katika mpango wa kumsajili Tyrique George kutoka Chelsea dirisha lililopita la majira ya kiangazi. Inaelezwa dili hilo lilisimama kwa changamoto ya kutofikia makubaliano juu ya ada ya uhamisho. George mwenyewe ndiye aliyekuwa akilazimisha sana kuondoka ili kupata muda mwingi zaidi wa kucheza tofauti na ilivyo katika kikosi cha Chelsea.


Emiliano Martinez

MANCHESTER United iliachana na mpango wa kumsajili kipa wa Aston Villa, Emiliano Martinez dakika za mwisho za dirisha la usajili na badala yake ikamgeukia kipa wa Royal Antwerp na Ubelgiji, Senne Lammens kwa ada ya Pauni 18 milioni. Martinez awali ndio alionekana kuwa chaguo la timu hiyo lakini inatajwa ada yake ya uhamisho na umri ndio tatizo.


Conor Gallagher

HADI dakika za mwisho za dirisha lililopita la usajili wa majira ya kiangazi, hakukuwa na uwezekano wa staa wa Atletico Madrid, Conor Gallagher kuondoka katika timu hiyo. Crystal Palace  ilikuwa na matumaini ya kumsajili staa huyu kabla dirisha hili halijafungwa usiku wa kuamkia leo na imekuwa ikimwinda tangu dirisha lililopita lakini changamoto ni Atletico haikuwa tayari kumuuza kwa sasa.