Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FBI yachunguza simu ya Rais wa Argentina

RAIS Pict

Muktasari:

  • Ndege iliyopangwa kuondoka saa 6:00 asubuhi iliondoka takribani saa 8:15, jambo lililosababisha kuchelewa kwa timu hiyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Ezeiza, ambako maelfu ya mashabiki walikuwa wakiisubiri.

NEW YORK, MAREKANI: RAIS wa Shirikisho la Soka Argentina (AFA), Claudio "Chiqui" Tapia, anadaiwa kushikiliwa kwa muda na maafisa wa FBI kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JFK, New York, muda mfupi kabla ya kupanda ndege kurejea Buenos Aires baada ya Kombe la Dunia.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Tapia alikuwa akisafiri pamoja na baadhi ya wajumbe wa ujumbe wa timu ya taifa ya Argentina alipodaiwa kuzungukwa na maafisa wa vyombo vya sheria vya Marekani na kutakiwa kukabidhi simu pamoja na vifaa vyake vya kielektroniki kwa ajili ya uchunguzi.

Vyanzo hivyo pia vilidai kuwa simu na kompyuta za baadhi ya wajumbe wengine wa msafara wa Argentina zilichukuliwa.

Ndege iliyopangwa kuondoka saa 6:00 asubuhi iliondoka takribani saa 8:15, jambo lililosababisha kuchelewa kwa timu hiyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Ezeiza, ambako maelfu ya mashabiki walikuwa wakiisubiri.

RAI 03

Hata hivyo, AFA imetoa taarifa rasmi ikikanusha madai hayo.

"Taarifa hizo si za kweli kabisa. Hakuna tukio lolote kati ya yaliyoelezwa lililotokea," ilisema taarifa ya shirikisho hilo.

RAI 01|

UCHUNGUZI WA FEDHA

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama zilizoripotiwa, waendesha mashtaka nchini Marekani wanachunguza madai kwamba mamia ya mamilioni ya dola za udhamini zinazohusishwa na AFA zilipitishwa kupitia benki za Marekani kwa njia inayoweza kuhusisha utakatishaji fedha na udanganyifu.

Wachunguzi wanataka kubaini fedha hizo zilielekezwa wapi, ni nani walizinufaika nazo na kama sheria za Marekani zilivunjwa.

Taarifa hizo zinadai Tapia anatakiwa kufika mbele ya Mahakama ya Wilaya ya Kusini ya Florida, pamoja na kuwasilisha taarifa zote alizonazo kuhusu kampuni ya Tourprodenter, ikiwemo mawasiliano yake na Pablo Toviggino, Diego Lucero na Javier Faroni.

RAI 02

Kampuni hiyo yenye makao yake Florida, inayosimamiwa na Faroni, inadaiwa kushughulikia malipo yaliyohusiana na baadhi ya mikataba mikubwa ya kibiashara ya AFA, ambayo sasa ipo chini ya uchunguzi.

Wachunguzi wanadai rekodi za benki zinaonyesha mamilioni ya dola yalipitishwa katika akaunti mbalimbali za taasisi za kifedha nchini Marekani, huku fedha nyingine zikibaki kwa muda mfupi kabla ya kuhamishwa kwenye akaunti nyingine.

Pia, inadaiwa kuwa uchunguzi umebaini malipo ya safari za ndege binafsi, usafiri, mafuta, huduma za ushauri pamoja na uhamishaji wa fedha kwa kampuni ambazo hazionekani kuwa na shughuli kubwa za kibiashara.

Katika taarifa hizo imeelezwa pia kuwa Lionel Messi hakuwa sehemu ya msafara uliokuwa unasafiri pamoja na Tapia.

Hata hivyo, ni muhimu kusisitiza kuwa AFA imekanusha madai hayo, na hadi sasa hayajathibitishwa na mamlaka za Marekani kupitia taarifa rasmi ya umma.