Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FA yamkomalia Infantino

FA Pict

Muktasari:

  • Infantino aliweka mfumo unaoruhusu rais wa FIFA kuhudumu kwa mihula mitatu pekee baada ya kuchukua nafasi ya Sepp Blatter mwaka 2016.

LONDON, ENGLAND: SHIRIKISHO la Soka England (FA) limewahi kutafakari uwezekano wa kupinga uhalali wa Gianni Infantino kugombea muhula wa nne wa urais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), lakini limebaini kuwa hatua hiyo huenda isifanikiwe.

FA pia limethibitisha kumuunga mkono mgombea mpinzani wa Infantino, Philippe Diallo, katika uchaguzi wa urais wa FIFA unaotarajiwa kufanyika Machi mwakani.

Infantino aliweka mfumo unaoruhusu rais wa FIFA kuhudumu kwa mihula mitatu pekee baada ya kuchukua nafasi ya Sepp Blatter mwaka 2016.

Hata hivyo, mwaka 2022, Baraza la FIFA lilikubaliana kuwa kipindi chake cha kwanza cha uongozi kati ya mwaka 2016 na 2019 hakitahesabiwa katika ukomo wa mihula mitatu. Uamuzi huo ulitokana na hoja kwamba Infantino alikamilisha tu kipindi cha mwisho cha mtangulizi wake, Blatter, ambaye alijiuzulu kabla ya kumaliza muda wake.

F 01

Mapema mwezi huu, taasisi ya kutetea haki za binadamu ya Fair Square iliandikia FA ikidai kuwa uamuzi huo unaweza kupingwa kisheria na kwamba unakinzana na madhumuni na dhamira ya katiba ya FIFA.

Taasisi hiyo iliitaka FA kuiomba Kamati ya Utawala ya FIFA kumzuia Infantino kugombea uchaguzi wa Machi, ikieleza kuwa tayari ametumikia mihula mitatu inayoruhusiwa.

Hata hivyo, mwenyekiti wa FA, Debbie Hewitt amejibu barua hiyo akieleza kuwa shirikisho hilo limechunguza uwezekano wa kupinga uhalali wa Infantino kugombea muhula mwingine, lakini halioni kama hatua hiyo inaweza kufanikisha lengo lililokusudiwa.

Katika mawasiliano yaliyoonekana na BBC, Hewitt amesema: “Mchakato uliofuatwa ulizingatia taratibu za utawala za FIFA na kufikia uamuzi wa kutohesabu kipindi cha sehemu ya muhula wa Infantino katika ukomo wa mihula ya urais.

F 02

“Baada ya kuchunguza kwa kina mchakato huo, hatuamini kuwa hatua ya kupinga uamuzi huo inaweza kufanikiwa.”

Kwa upande wake, Fair Square imesema inaelewa kwa nini FA haina imani na mifumo ya ndani ya FIFA katika kuwawajibisha viongozi wanaokiuka kanuni, lakini imeonya kuwa kuachana na njia hizo ni kosa kwa sababu kunampa Infantino ishara kwamba anaweza kufanya atakavyo.