Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dumfries azichanganya Man United, Man City

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Dumfries ana mkataba na Inter Milan hadi Juni 2026 na taarifa zinaeleza kuwa timu yake inahitaji takriban Euro 30 milioni ili kumuuza ifikapo Januari, mwakani.

MANCHESTER United ipo tayari kushindana na Manchester City kwa ajili ya kumsajili beki wa kulia wa Inter Milan, Denzel Dumfries, mwenye umri wa miaka 29, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Dumfries ana mkataba na Inter Milan hadi Juni 2026 na taarifa zinaeleza kuwa timu yake inahitaji takriban Euro 30 milioni ili kumuuza ifikapo Januari, mwakani.

Mbali ya Man United na Man City, saini ya beki huyo pia iliwahi kuhitajika na Liverpool ambayo ilihusishwa kumsajili  katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi, lakini baadaye iliachana na mpango huo na kuchagua kumfuatilia Jeremie Frimpong kutoka Bayer Leverkusen.

Dumfries alikuwa na kipengele kinachomruhusu kuondoka ikiwa timu inayomhitaji italipa Pauni 21.5 milioni, lakini kilikuwa kinadumu kabla ya Julai 15 ambapo baada ya hapo Inter ilikuwa na haki ya kutaka kiasi chochote kwa timu inayomtaja.

Inter italazimika kumuuza katika dirisha lijalo ikiwa hatasaini mkataba mpya kwani ifikapo majira ya kiangazi mwakani atakuwa mchezaji huru. Msimu uliopita alicheza mechi 28 za michuano yote.


Luis Benedetti

ARSENAL, Barcelona na Napoli zinainyemelea saini ya beki wa kati wa Palmeiras, Luiz Gustavo Benedetti, mwenye umri wa miaka 19. Fundi huyo wa kimataifa wa Brazil ni mmoja kati ya vipaji vilivyoibukia nchini Brazil na msimu uliopita  inaelezwa kwamba timu yake inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 30 milioni ili kumuuza. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo unatarajiwa kumalizika 2029.


Elliot Anderson

MANCHESTER United inamfuatilia kiungo wa kati wa Nottingham Forest, Elliot Anderson, mwenye thamani ya karibu Pauni 70 milioni. Lakini, mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 22 bado ana furaha ya kuendelea kusalia Nottingham. Anderson amekuwa mhimili wa safu ya kiungo ya Nottingham msimu huu. Mkataba wake na timu hiyo unatarajiwa kumalizika 2028, na mbali ya Man United saini yake pia inahitajika na Newcastle United.


Kenan Yildiz

JUVENTUS inapambana kumsainisha mkataba mpya mshambuliaji wa kimataifa wa Uturuki, Kenan Yildiz mwenye umri wa miaka 20 ambaye katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi alikataa ofa ya Chelsea ya Pauni 70 milioni. Yildiz alicheza mechi 34 msimu uliopita katika Serie A, akifunga mabao manane na kutoa asisti sita. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2029.


Adam Wharton

CRYSTAL Palace inaweza kuzingatia ofa kuanzia Pauni 60 milioni kwa ajili ya kumuuza kiungo wa kimataifa wa England, Adam Wharton katika dirisha lijalo la majira ya baridi ambapo Liverpool imeonyesha nia ya kutaka kumsajili. Wharton mwenye umri wa miaka 21, alijiunga na Palace kutoka Blackburn Rovers 2024 kwa ada ya takriban Pauni 18 milioni. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2029.


Jeremy Monga

REAL Madrid inamfuatilia winga chipukizi wa Leicester City, Jeremy Monga, mwenye umri wa 16, anayekichezea kikosi cha vijana cha England kwa wachezaji wenye umri wa miaka 19. Monga ni miongoni mwa wachezaji wenye kasi na uwezo wa kumiliki mpira. Vilevile amekuwa akilinganishwa na Jadon Sancho katika mbinu zake za kiuchezaji. Msimu huu amecheza mechi nne za michuano yote na kufunga bao moja.


Jorthy Mokio

LIVERPOOL na Manchester United zinaendelea kupigana vikumbo kuwania saini ya kiungo wa kati wa Ajax, Jorthy Mokio, 17, ambaye tayari ameshacheza na timu taifa ya Ubelgiji. Kinda huyo mwenye uwezo wa kucheza kama beki na kiungo wa kati ni miongoni mwa vipaji vilivyoibuliwa na Ajax inayodaiwa kuwa tayari kumuuza, lakini kwa kiasi cha pesa kisichopungua Pauni 40 milioni.


Marc Bernal

CHELSEA inaonekana kuwekeza nguvu zaidi katika mpango wa kutaka kumsajili kiungo wa Barcelona na timu ya taifa ya vijana ya Hispania, Marc Bernal, 18, dirisha lijalo baada ya kushindwa kumpata katika dirisha lililopita la majira ya baridi. Kiungo huyo ilishindikana kuondoka katika dirisha lililopita kutokana na majeraha aliyokuwa nayo. Timu zote tatu zinapanga kufanya kila liwezekanalo ili kumpata Januari.