Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dominic Solanke mlangoni Spurs

Muktasari:

Staa huyo mwenye miaka 26 amesaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo hadi mwaka 2030 huku kocha Ange Postecoglou akisifu usajili huo.

London, England: Klabu ya Tottenham imekiri kumsajili mshambuliaji Dominic Solanke kutoka kwenye kikosi cha Bournemouth baada ya msimu uliopita kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu England.

Staa huyo mwenye miaka 26 amesaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo hadi mwaka 2030 huku kocha Ange Postecoglou akisifu usajili huo.

Staa huyo amesajiliwa kwa kitita cha pauni 65 milioni akiwa msimu uliopita alifanikiwa kufunga mabao 19 na kuisaidia Bournemouth kumaliza kwenye nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi.

Awali staa huyo alikuwa akiwindwa na timu kadhaa kubwa ikiwemo Liverpool ambayo mwanzoni mwa kipindi cha usajili ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kumpata mchezaji huyo.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool anatajwa kama mmoja kati ya wachezaji mahiri zaidi kwenye ligi hiyo

Solanke alikuwa kwenye kikosi cha England kilichoshiriki michuano ya Euro mwaka huu lakini alikosa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza akiwa nyuma ya Ollie Watkins, Ivan Toney na Harry Kane.