Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Doku: Nikiongeza tu mabao nakuwa winga bora duniani

DOKU Pict

Muktasari:

  • Katika nusu fainali ya FA itakayochezwa leo, Jumamosi, katika Uwanja wa Wembley, kazi ya Southampton itakuwa kumdhibiti winga huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ambaye ameboresha zaidi kiwango chake msimu huu.

LONDON, ENGLAND: ANAJISIFU? Bila shaka ana kitu miguuni mwaka. Kasi, nguvu ya kushambulia na ustadi wa haraka wa kupiga chenga, winga wa Manchester City, Jeremy Doku ni jinamizi kwa mabeki wa timu pinzani katika Ligi Kuu England na Ulaya.

Katika nusu fainali ya FA itakayochezwa leo, Jumamosi, katika Uwanja wa Wembley, kazi ya Southampton itakuwa kumdhibiti winga huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ambaye ameboresha zaidi kiwango chake msimu huu.

DOK 04

Kocha wa Liverpool, Arne Slot, anaamini kuwa Doku “hawezi kuzuilika”, na beki wa Arsenal, Cristhian Mosquera alijionea hilo katika ushindi wa mabao 2-1 wa Man City kwenye Ligi Kuu England alipolazimika kumchezea faulo mara kwa mara hadi kuonywa kwa kadi ya njano katika Uwanja wa Etihad.

Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 haridhiki. Anataka kuongeza mabao kwenye uwezo wake ili ajikite juu ya Vinicius Junior wa Real Madrid kama winga bora zaidi duniani. Akiwa amefunga mabao manne katika mechi 40 za Man City msimu huu, hiyo ni chini ya kiwango chake hasa ukilinganisha na mabao 18 ya Vinícius katika mechi 48 akiwa na Real Madrid.

Lakini, je, anaweza kufikia kiwango hicho? “Bila shaka,” anasema Doku.

DOK 03

“Nahisi nikiongeza mabao, mazungumzo yatabadilika kabisa. Kuhusu pasi za mabao niko vizuri. Nahitaji kuwa mara nyingi zaidi katika maeneo ya kufunga mabao kwa urahis. Mabao ya kugusa tu mpira. Nikitazama mabao yangu hata msimu huu mengi yanatokana na chenga. Nataka kufunga hata mabao matano ya aina hiyo kwa msimu. Winga anahitaji kufunga. Nikifanya hivyo, naamini ninaweza kuwa bora duniani kwa asilimia 100.”

Hadi sasa ana asisti 11 katika mashindano yote, akilinganishwa na tisa katika kila moja ya misimu yake miwili ya kwanza Man City. Alifunga mabao sita katika msimu wake wa kwanza 2023-24 na nane uliopita, ikiwemo mawili katika Kombe la Dunia la Klabu. Mwanzoni mwa maisha yake ya soka alikuwa mshambuliaji wa kati.

“Nilikuwa namba tisa nikiwa na miaka tisa au 10. Baadaye nikawa winga kuanzia kama miaka 12. Nilipenda kuwaangalia Neymar Jr, Lionel Messi, Franck Ribery, Eden Hazard, Arjen Robben na Ronaldinho. Kisha nikatengeneza mtindo wangu mwenyewe. Siwezi kufanya wanachofanya wao, na wao hawawezi kufanya ninachofanya mimi. Najitahidi kutumia ubora wangu,” anasema mchezaji huyo.

DOK 02

Kuhusu kasi yake, anasema: “Siku zote nimekuwa na kasi. Ndugu yangu alikuwa na kasi, baba yangu pia, hivyo ni kitu cha kifamilia. Nafikiri mimi na Abdukodir Khusanov ndio wenye kasi zaidi kikosini. Kwa mita 15, najiona bora. Lakini kwa mita 40, huenda yeye akanishinda.”

Maoni ya Slot kuhusu Doku yalikuja baada ya kuivuruga Liverpool katika ushindi wa mabao 4-0 kwenye Kombe la FA, ambapo mchango wake upande wa kushoto ulikuwa muhimu kwa hat-trick ya Erling Haaland.

Sifa nyingine ilionekana wakati Trent Alexander-Arnold alipoonekana kuiga mtindo wa chenga wa Doku baada ya Real Madrid kuwaondoa Man City kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi Machi. “Niliona ile video. Ilikuwa pambano zuri dhidi yake,” anasema Doku.

DOK 01

“Nikicheza sasa, mara nyingi nakabiliwa na mabeki wawili, jambo ambalo si tatizo kwa sababu linaacha mchezaji mwingine huru. Lakini najua moja kwa moja dhidi ya mmoja hapo ndipo nguvu yangu kubwa ilipo.”

Leo, Jumamosi atajaribu kuonyesha hilo kuisaidia City kufika fainali ya nne mfululizo ya FA. Ikiwa kikosi cha Pep Guardiola kitafanikiwa kuwatoa Southampton, Doku anataka matokeo tofauti na kushindwa kwao dhidi ya Crystal Palace na Manchester United katika fainali mbili zilizopita.

“Matokeo hayo yanabaki kichwani, lakini najitahidi kutoangalia vitu nisivyokuwa navyo. Nashukuru kwa nilichoshinda tayari. Sasa tuko nusu fainali, nataka kufika fainali na kushinda kombe hilo. Nimeshashinda Carabao na Ligi Kuu England, sasa nataka kushinda FA pia.”