Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Deco ampa Lamine Yamal Ballon D'or

YAMAL Pict

Muktasari:

  • Yamal, mwenye umri wa miaka 19, alishika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro cha tuzo hiyo mwaka uliopita baada ya kuzidiwa kidogo tu na mshambuliaji wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Ufaransa, Ousmane Dembele.

BARCELONA, HISPANIA: MKURUGENZI wa michezo wa Barcelona, Deco amesema Lamine Yamal ndiye anayestahili kuwa kipenzi namba moja cha kutwaa tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu, huku akionyesha kushtushwa na hatua ya kutojumuishwa kwa nyota wengine wa klabu hiyo, Raphinha na Pedri, katika orodha ya walioteuliwa akitaja uamuzi huo kuwa ni “kashfa kubwa”.

Yamal, mwenye umri wa miaka 19, alishika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro cha tuzo hiyo mwaka uliopita baada ya kuzidiwa kidogo tu na mshambuliaji wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Ufaransa, Ousmane Dembele.

Kinda huyo anayeendelea kuteka hisia za walimwengu amekuwa na mwaka mwingine wa mafanikio makubwa baada ya kuisaidia Barcelona kutwaa ubingwa wa LaLiga, pamoja na kuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Hispania kilichotwaa Ubingwa wa Dunia.

Kupitia mafanikio hayo, Yamal ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mdogo kucheza fainali za Mashindano ya Ulaya (Euro) na Fainali za Kombe la Dunia akiwa kijana mdogo, kufuatia kutwaa Ubingwa wa Euro 2024 miaka miwili iliyopita akiwa na La Roja.

YAMA 01

Takwimu zinaonyesha mshambuliaji huyo alikamilisha chenga nyingi zaidi katika ligi kuu tano za Ulaya msimu uliopita (133). Katika mwaka huu wa kalenda, ni Harry Kane (43) na Michael Olise (34) pekee waliomzidi Yamal katika kuhusika kwenye mabao mengi ya moja kwa moja na amehusika kwenye mabao 29 (akifunga mabao 20 na kutoa asisti tisa).

Pia, kinda huyo ndiye kinara wa kutengeneza nafasi za mabao katika ligi hizo kubwa msimu huu akiwa tayari ametengeneza nafasi 22. Kutokana na kiwango hicho, Deco anaamini hakupaswa kuwa na shaka kuhusu nani anayestahili tuzo hiyo.

“Nadhani Lamine ndiye kipenzi namba moja, bila shaka kabisa,” amesema Deco alipokuwa akizungumza na kituo cha redio cha RAC1.

“Si tu kwa sababu ya kile alichokifanya akiwa na Barcelona, bali pia ametwaa Kombe la Dunia akiwa mchezaji muhimu wa Hispania.”

YAMA 02

Deco ameongeza: “Tusisahau pia aliingia kwenye Fainali za Kombe la Dunia akiwa anatoka kwenye majeraha. Alikuwa mchezaji bora zaidi wa LaLiga msimu uliopita. Sisemi hivi kwa sababu Lamine ni mchezaji wetu, bali kwa sababu napenda soka la kweli.”

Mbali na hayo, Deco hakusita kueleza kukasirishwa kwake na kitendo cha wachezaji wenzake na Yamal ndani ya Barcelona, Raphinha na Pedri, kuachwa kwenye orodha ya wanaowania tuzo hiyo, licha ya Pedri pia kuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa Kombe la Dunia.

“Kwake mimi, hiyo ni kashfa kubwa,” ameongeza Deco. “Sielewi kabisa orodha hizi zinavyotengenezwa. Kumuona Pedri hayupo, pamoja na kipaji kikubwa alichonacho... kweli sielewi kabisa.”