Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cristiano Ronaldo bado tishio, afunga mwaka na rekodi yake

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo aliifungia mabao mawili Al-Nassr katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Al Akhdoud Jumamosi mchana, na kufanya jumla ya mabao yake kufikia 956.

LISBON, URENO: STAA wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo amefikisha bao lake la 40 mwaka huu na kuendelea kusogea karibu na ndoto yake ya kufunga mabao 1,000 katika maisha yake ya soka.

Nyota huyo aliifungia mabao mawili Al-Nassr katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Al Akhdoud Jumamosi mchana, na kufanya jumla ya mabao yake kufikia 956.

Baada ya kufunga mabao hayo, Ronaldo aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa X akisema kufanya kazi kwa bidii ndio njia ya mafanikio.

Ronaldo  mwenye umri wa miaka 40  mwaka wake bora zaidi katika maisha yake ya soka ulikuwa ni mwaka 2013, alipofunga mabao 63 katika mashindano yote kwa klabu na timu ya taifa.

Fundi huyu anaonekana kuwa  bado yuko katika hali nzuri sana kimwili licha ya umri kumtupa mkono  na hivi karibuni aliposti picha yake akiwa bila shati, akionyesha mwili wake ulivyojengeka.

Katika mahojiano yake na Piers Morgan mwezi uliopita, Ronaldo amesema anaamini atacheza kwa mwaka mmoja au miwili zaidi kabla ya kustaafu.

Inaelezwa Ronaldo, anafanya mazoezi kwa saa tatu hadi nne kwa siku, pia katika chakula staili ya fundi huyu upo tofauti.

Ronaldo hupendelea kula milo sita kwa siku akianza na kifungua kinywa, brunch, chakula cha mchana, vitafunwa, supper na chakula cha jioni.

Mbali ya kutaka kufikisha mabao 1000, Ronaldo pia ana malengo ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia nchini Marekani mwakani.

Katika msimu huu, fundi huyu amefunga mabao 12 katika mechi tisa za michuano yote akiwa na Al Nassr.