Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cristian Romero aaga Spurs

Muktasari:

  • Atletico wamekubaliana kwa kanuni juu ya dili lenye thamani ya pauni 34 milioni kwa ajili ya beki huyo.

LONDON, ENGLAND; NAHODHA wa Tottenham, Cristian Romero, amewaaga mashabiki wa klabu hiyo kabla ya kuthibitisha uhamisho wake kwenda Atletico Madrid.

Atletico wamekubaliana kwa kanuni juu ya dili lenye thamani ya pauni 34 milioni kwa ajili ya beki huyo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina aliandika ujumbe wa kuaga kupitia Instagram akisema:

“Leo, naaga mahali ambapo kwa misimu mitano haikuwa tu klabu. Ilikuwa nyumba yangu, changamoto yangu na mahali ambapo mimi na familia yangu tulijenga sehemu muhimu sana ya maisha yetu.

“Naondoka nikiwa na moyo uliojaa kumbukumbu na fahari kubwa kwa kila kitu tulichoishi na kufanikisha pamoja.

“Nilipofika, nilikuwa na ndoto iliyo wazi: kuacha jina langu katika historia ya klabu hii. Nilijua njia pekee ya kufanya hivyo ilikuwa kupitia kufanya kazi kwa bidii, kujitoa na kufanikisha jambo ambalo lilionekana kuwa gumu sana kwa muda mrefu: kushinda tena taji.

“Safari haikuwa kamilifu, lakini sitaki hilo ndilo lifafanue kuaga kwangu. Nachagua kukumbuka nyakati za furaha, mafunzo, watu waliosimama pamoja nami na, zaidi ya yote, upendo nilioupokea katika miaka hii mitano.

“Asanteni kila mtu ndani ya klabu aliyeshiriki safari hii pamoja nami. Makocha, wachezaji wenzangu, wafanyakazi na kila mtu aliyekuwa akifanya kazi nyuma ya pazia — nyote ni sehemu ya hadithi yangu na mna nafasi katika moyo wangu.

“Na kwa mashabiki: Asanteni kwa kunipenda, kuniheshimu na kunifanya nijisikie kama mmoja wenu tangu siku ya kwanza. Asanteni kwa kila kumbatio, kila wimbo, kila bendera, kila makofi na kwa kuwa nami daima.

“Najua sikuwa mkamilifu, lakini jambo moja linanipa amani: siku zote nilitoa kila kitu. Niliilinda jezi hii kwa fahari na kwa moyo wangu wote.

“ASANTENI KWA KILA KITU. Naondoka klabuni, lakini sehemu ya moyo wangu itabaki hapa milele.

“Wakati mmoja nilikuwa mmoja wenu. Leo, naondoka nikiwa mmoja wenu milele.

“Kwa upendo na heshima zangu zote.”

Gazeti la Daily Mail Sport, liliripoti kuwa mabingwa wa Ligi Kuu England, Arsenal, waliwasiliana na mawakala wa nahodha huyo wa Spurs kuhusu masharti ya dili hilo.

Hata hivyo, Tottenham hawakuwa na taarifa kuhusu nia ya Arsenal na hawakuwa tayari kumuuza Romero mwenye umri wa miaka 28 kwa wapinzani wao wa kaskazini mwa London.

Beki huyo wa kati alikuwa huru kuondoka Tottenham kwa bei inayofaa baada ya klabu hiyo kuimarisha safu yake ya ulinzi mapema katika dirisha la usajili.

Usajili wa Marcos Senesi kwa uhamisho wa bure pamoja na Jan Paul van Hecke kutoka Brighton kwa pauni milioni 52 unamaanisha kwamba Roberto De Zerbi sasa ana chaguo la kutosha katika safu ya ulinzi kwa msimu unaokuja.