Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bayern Munich yaziita mezani PSG, Liverpool dili la Olise

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Olise, ambaye alijiunga na Bayern akitokea Crystal Palace mapema mwaka jana kwa takribani Euro 60 milioni, amekuwa akihusishwa na klabu kadhaa kubwa ikiwemo Liverpool, Manchester City na Paris Saint-Germain.

MKURUGENZI wa michezo wa Bayern Munich, Max Eberl amethibitisha winga wao wa kimataifa wa Ufaransa, Michael Olise,23, hana kipengele cha kuvunja mkataba katika mkataba wake utakaomalizika mwaka 2029, hivyo timu yoyote inayohitaji saini yake itatakiwa kuwasilisha ofa mezani ili waijadili.

Olise, ambaye alijiunga na Bayern akitokea Crystal Palace mapema mwaka jana kwa takribani Euro 60 milioni, amekuwa akihusishwa na klabu kadhaa kubwa ikiwemo Liverpool, Manchester City na Paris Saint-Germain.

Licha ya kuwa tayari kuziita mezani timu zinazomhitaji fundi huyo, taarifa zinaeleza Olise ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa Bayern, hivyo haitokuwa rahisi kumwachia.

Baadhi ya ripoti zinadai Bayern inaweza kuhitaji takribani Euro 150 milioni kama ada ya uhamisho ya fundi huyo.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Olise amecheza mechi 17 za michuano yote, amefunga mabao tisa na kutoa asisti nane.


Angelo Stiller

MANCHESTER United imeonyesha nia ya kumsajili kiungo mkabaji wa VfB Stuttgart, Angelo Stiller,24, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Kwa mujibu wa Sky Sports Germany, Stuttgart inahitaji zaidi ya Euro 50 milioni ili kumuuza  mchezaji huyo. Stiller, aliyepitia katika akademi ya Bayern Munich, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Elliot Anderson

NEWCASTLE United inaripotiwa kuchunguza uwezekano wa kumsajili kiungo wake wa zamani, raia wa England, Elliot Anderson, 22, ambaye ilimuuza kwenda Nottingham Forest mwaka 2024. Kwa mujibu wa gazeti la i Paper, Newcastle inavutiwa na kutaka kumrejesha mchezaji huyo kutokana na kiwango bora alichoonyesha msimu huu akiwa Forest na amekuwa mchezaji muhimu eneo la kati kwa kasi yake.


Conor Gallagher

KWA mujibu wa tovuti ya Football Insider, Atletico Madrid iko tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kumuuza kiungo wao wa kimataifa wa England, Conor Gallagher,25, anayehusishwa pia na Manchester United. Man United inamwona Gallagher kama mbadala sahihi wa Kobbie Mainoo ambaye kocha Ruben Amorim hamhitaji.


Harry Maguire

BEKI wa kati wa Manchester United, Harry Maguire anaweza kuondoka Manchester United bure mwishoni mwa msimu ujao baada ya mkataba wake kumalizika mwisho wa msimu huu. Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Mail, hadi sasa Man United haijaamua kama itamwongezea mkataba beki huyo,32, ambaye alijiunga na klabu hiyo mwaka 2019 kutoka Leicester City kwa dau kubwa la Pauni 80 milioni.


Fikayo Tomori

MABOSI wa AC Milan wanaendelea kufanya mazungumzo na wakala wa Beki wa England Fikayo Tomori juu ya kumwongeza mkataba mpya. Kwa mujibu wa ripoti za mwandishi mashuhuri Fabrizio Romano, Tomori, 27, kipaumbele chake cha kwanza ni kuendelea kusalia Milan. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Samuel Omorodion

ASTON Villa na Newcastle United zimeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa FC Porto, Samuel Omorodion, 21. Villa na Newcastle zinafuatilia kwa karibu maendeleo ya Omorodion, ambaye kila siku amezidi kuimarika. Omorodion ambaye ana asili ya Nigeria lakini amechagua kuichezea Hispania, alikaribia kujiunga na Chelsea msimu uliopita kabla ya dili kufeli.


Jean-Philippe Mateta

MSHAMBULIAJI wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Ufaransa Jean-Philippe Mateta, mwenye umri wa miaka 28, anadaiwa kutaka kuondoka Crystal Palace katika dirisha lijalo ambapo klabu kama Manchester United, Newcastle United, na Tottenham Hotspur zinaonekana kutaka kumsajili. Kwa mujibu wa Caught Offside, Mateta anataka kupata changamoto mpya sehemu nyingine.