Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea yamsubiri Enzo Fernandez

Muktasari:

  • Hata hivyo, Manchester City haimthamini kiungo huyo kwa bei ya pauni 120 milioni ambayo Chelsea imeweka.

LONDON, ENGLAND; KOCHA mpya wa Manchester City, Enzo Maresca amekuwa akitamani kukutana tena na kiungo wa kimataifa wa Argentina, Enzo Fernandez, katika kikosi chake cha The Etihad.

Hata hivyo, Manchester City haimthamini kiungo huyo kwa bei ya pauni 120 milioni ambayo Chelsea imeweka.

Fernandez, mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akionesha wazi tangu Machi mwaka huu kwamba anatamani kuondoka, huku wakala wake, Javier Pastore, pia akizungumzia hadharani uwezekano wa mchezaji huyo kuondoka Stamford Bridge.

Chelsea iliwasilisha kwa kambi ya mchezaji huyo masharti yaliyokuwa yanakubalika, ikiwemo ada ya pauni 120 milioni 120 pamoja na mfumo wa malipo uliowafaa, mwanzoni mwa dirisha la usajili.

Hata hivyo, kwa kuwa muda wa mwisho wa makubaliano hayo sasa umepita, masharti hayo kwa mujibu wa watu wa ndani ya klabu hayapo tena mezani, na kiungo huyo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Xabi Alonso kwa msimu mzima.

Chelsea haiko tayari kumuuza katika dirisha la Januari.

Kocha mpya Alonso alisema wakati wa kutambulishwa kwake mwezi uliopita kwamba anataka kumbakiza nyota huyo wa zamani wa Benfica katika klabu hiyo.

Real Madrid pia ilifikiria kumsajili Fernandez mwanzoni mwa dirisha la usajili, kabla ya kutoa taarifa rasmi kwamba haitafuatilia dili hilo.

Fernandez alikuwa akitajwa kama mmoja wa wachezaji waliokuwa wakifikiriwa kuchukua nafasi ya Rodri huko Manchester City, huku kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania akiwa anakaribia kuhamia Real Madrid.

Hata hivyo, alipoulizwa Ijumaa kama Manchester City ingekidhi muda wa mwisho uliowekwa na klabu yake ya zamani, Maresca alisema:

“Kwa uaminifu, si leo. Sidhani kama tutafanya jambo lolote leo.

“Kwa hakika kuna mambo tunayohitaji kufanya, ni mangapi sijui. Inaweza kuwa moja, inaweza kuwa mawili, inategemea pia kama wachezaji wanataka kuondoka, hivyo tutaona.

“Ni saa 48 kabla ya fainali, fainali yangu ya kwanza katika klabu hii.

“Ningependa kushinda taji langu la kwanza, kwa hiyo mawazo yangu hayapo kwa wachezaji wanaoweza kuondoka au wanaoweza kuja. Mawazo yangu yako kwenye mchezo.”