Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea yaizidi Arsenal kwa Morgan Rogers

ROGERS Pict

Muktasari:

  • Rogers alikuwa mmoja wa malengo makubwa ya Arsenal katika dirisha lote la usajili wa majira ya kiangazi. Hata hivyo, hadi sasa mabosi wa Arsenal walishindwa kufikia kiwango cha fedha kilichokuwa kikihitajika na Aston Villa ili kumuachia nyota huyo.

LONDON, ENGLAND: CHELSEA inatarajiwa kukamilisha usajili wa kushangaza wa mshambuliaji Morgan Rogers kutoka Aston Villa kwa ada ya pauni 117 milioni wiki hii, katika dili litakaloweka rekodi mpya ya usajili wa mchezaji wa Uingereza ndani ya Ligi Kuu England.

Rogers alikuwa mmoja wa malengo makubwa ya Arsenal katika dirisha lote la usajili wa majira ya kiangazi. Hata hivyo, hadi sasa mabosi wa Arsenal walishindwa kufikia kiwango cha fedha kilichokuwa kikihitajika na Aston Villa ili kumuachia nyota huyo.

Arsenal ilikuwa ikiamini kuwa ipo kwenye nafasi nzuri ya kumsajili Rogers, ambaye inaelezwa alikuwa tayari kujiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu. Lakini ndani ya klabu hiyo kuliaminika kuwa walichelewa kuchukua hatua, licha ya kocha Mikel Arteta kuwa tayari alikutana na mchezaji huyo. Aston Villa pia haikuridhishwa na mwendo wa mazungumzo kutoka kwa Arsenal.

ROG 01

Kwa mujibu wa Daily Mail Sport, Chelsea sasa imeingia rasmi kwenye mbio hizo na ina matumaini makubwa ya kukamilisha dili la pauni 117 milioni, sawa na shilingi bilioni 114 .

Rogers anaweza kufanyiwa vipimo vya afya mapema leo mara baada ya kurejea kutoka Marekani akiwa na kikosi cha England, kabla ya kuweka saini mkataba wa miaka sita ndani ya Stamford Bridge.

Licha ya Arsenal kuendelea kumkubali sana Rogers, bado pia wanaendelea kumfuatilia winga wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Ufaransa, Bradley Barcola, ambaye yupo juu kwenye orodha yao ya usajili.

ROG 02

Mkuu wa kitengo cha kutambua vipaji wa Chelsea, Joe Shields, anamfahamu Rogers tangu kipindi walipokuwa Manchester City. Wawili hao waliwahi kufanya kazi pamoja, huku Rogers pia akicheza sambamba na nyota wa sasa wa Chelsea, Cole Palmer na Tosin Adarabioyo.

Ingawa Aston Villa itashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu huku Chelsea ikikosa nafasi ya kushiriki michuano yoyote ya Ulaya, taarifa zinaeleza kuwa suala hilo halitakuwa na ushawishi mkubwa katika uamuzi wa Rogers.

ROG 03

Mbali na Rogers, Arsenal pia imeonyesha nia ya kumsajili beki wa Aston Villa, Ezri Konsa. Ofa rasmi inatarajiwa kutumwa, ingawa bado kuna tofauti kubwa ya tathmini ya thamani ya mchezaji huyo kati ya pande hizo mbili.

Iwapo Rogers ataondoka majira haya ya kiangazi, Aston Villa itapoteza mmoja wa wachezaji wake muhimu ambaye amefikisha mabao na pasi za mabao zenye idadi ya tarakimu mbili katika misimu miwili iliyopita.

Kutokana na Villa kulazimika kuendesha matumizi kwa umakini baada ya kukiuka kanuni za matumizi za UEFA, mauzo hayo ya rekodi yataimarisha hali ya kifedha ya klabu na kumpa kocha Unai Emery nafasi ya kufanya usajili mwingine.