Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea inaongoza matumizi ya pesa EPL!

CHELSEA Pict

Muktasari:

  • Mabingwa hao wa dunia wamefanya vyema pia kwenye Ligi Kuu England, wakinyakua taji hilo mara tano, ikiwa ni sehemu ya kufurahia kuongoza kwa matumizi makubwa.

LONDON, ENGLAND: NDO hivyo. Chelsea ndiyo timu iliyofanya matumizi makubwa ya pesa kwenye Ligi Kuu England kuliko timu nyingine zote na imezizidi klabu wapinzani kwa pesa nyingi sana.

Mabingwa hao wa dunia wamefanya vyema pia kwenye Ligi Kuu England, wakinyakua taji hilo mara tano, ikiwa ni sehemu ya kufurahia kuongoza kwa matumizi makubwa.

The Blues ilitumia Pauni 1.3 bilioni kwa kipindi cha miaka mitatu tangu ilipochukuliwa na bilionea Todd Boehly. Na hilo ndilo lililowafanya kushika namba moja kwenye timu zilizofanya matumizi makubwa kwenye usajili kwenye Ligi Kuu England.

Kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi imemsajili Joao Pedro, Liam Delap na Jamie Gittens na kufanya matumizi ya Chelsea kufikia Pauni 4 bilioni, kwa mujibu wa Transfermarkt.

Hiyo ina maana, Chelsea imetumia Pauni 1 bilioni zaidi ya timu inayoshika nafasi ya pili kwenye matumizi, Manchester City. Na miamba hiyo ya Etihad, imewazidi mahasimu wao na majirani zao, Manchester United kwa tofauti ya Pauni 300 milioni.

Man City imefanya matumizi makubwa tangu 2008, wakati Sheikh Mansour alipoinunua klabu hiyo. Man City imetumia Pauni 3.1 bilioni, wakati Man United imetumia Pauni 2.8 bilioni, huku klabu nyingine za Big Six zikiingia ndani ya Top Six ya matumizi.

Liverpool, Arsenal na Tottenham zote zimevuka matumizi ya Pauni 2 bilioni, huku usajili wa Florian Wirtz, Jeremie Frimpong na Milos Kerkez waliotua Anfield, umewafanya wawe juu ya Arsenal katika matumizi.

Tottenham matumizi yao ya Pauni 2 bilioni yamewafanya kushika nafasi ya sita, huku Everton, Newcastle, West Ham na Aston Villa zikifanya matumizi ya Pauni 1.3 bilioni.

Kwenye 10 bora ya matumizi ya timu, hakuna hata moja iliyotumia chini ya Pauni 1 bilioni. Brighton na Bournemouth zimeingia kwenye orodha ya timu zilizofanya matumizi makubwa licha ya kuwapo kwenye Ligi Kuu England mwaka 2017 na 2015 mtawalia.

Wakati Nottingham Forest matumizi makubwa tangu iliporejea kwenye Ligi Kuu England 2022 ikishika namba 20 kwenye timu zilizofanya matumizi makubwa.

Kuhusu Chelsea, yenyewe imefanya usajili wa mastaa wawili kwa ada zinazozidi Pauni 100 milioni, Enzo Fernandez na Moises Caicedo, huku Romelu Lukaku na Mykhailo Mudryk ambao pia dili zao zilikuwa za pesa nyingi.

Na matumizi ya Chelsea yalianza tangu alipokuja bilionea Roman Abramovich mwaka 2003, lakini pesa imetumika maradufu zaidi ilipoanza kumilikiwa na bilionea Boehly.

Man City nayo imeendelea kuonyesha nguvu yake kwenye matumizi, ikiwamo kufanya usajili wa Pauni 203 milioni kwenye dirisha la Januari kabla ya matumizi ya Pauni 102M dirisha la kiangazi.