Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carragher amlaumu Mathys Tel, Roberto De Zerbi ampinga

SPURS Pict

Muktasari:

  • Mfaransa huyo alikuwa njiani kuwa shujaa wa mechi baada ya kuifungia Spurs bao la kuongoza mapema kipindi cha pili kwa shuti kali lililopinda vizuri. Ushindi huo ungeiweka timu hiyo ya kocha Roberto De Zerbi alama nne mbele ya West Ham zikiwa zimesalia mechi mbili pekee.

MCHAMBUZI wa soka, Jamie Carragher amemkosoa vikali mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Mathys Tel, kufuatia uamuzi wake wa kupiga mpira wa ‘sarakasi’ uliosababisha penalti na kuwanyima Spurs ushindi katika sare ya 1-1 dhidi ya Leeds United.

Mfaransa huyo alikuwa njiani kuwa shujaa wa mechi baada ya kuifungia Spurs bao la kuongoza mapema kipindi cha pili kwa shuti kali lililopinda vizuri. Ushindi huo ungeiweka timu hiyo ya kocha Roberto De Zerbi alama nne mbele ya West Ham zikiwa zimesalia mechi mbili pekee.

‘Maafa’ yalitokea pale Tel alipojaribu kuondoa hatari ndani ya eneo la Tottenham kwa mtindo wa ‘sarakasi’, na badala yake akampiga teke la kichwa mchezaji wa Leeds, Ethan Ampadu.

SPU 01

Baada ya mwamuzi, Jarred Gillett kupata usaidizi wa marudio ya video (VAR), alitoa penalti ambayo ilifungwa kwa umakini na Dominic Calvert-Lewin.

Akizungumza kwenye kipindi cha ‘Monday Night Football’, Carragher ameeleza kusikitishwa kwake akisema: "Ni uamuzi wa kichaa kabisa kutoka kwa Tel. Alimwona mchezaji wa pinzani akija lakini bado akaamua kupiga. Alikuwa na muda wa kubadili mawazo yake lakini hakufanya hivyo. Ni uamuzi mbovu sana kutoka kwa mchezaji kijana wa safu ya ushambulizi."

Licha ya makosa hayo, kocha wa Tottenham Roberto De Zerbi amekataa kumlaumu hadharani mchezaji huyo mwenye umri mdogo na badala yake alimtetea.

SPU 02

De Zerbi amesema hatamfokea bali atamkumbatia na kumbusu Tel, huku akisisitiza kuwa mchezaji huyo ni kijana mwenye kipaji kubwa na makosa kama hayo hutokea katika soka.

Ameongeza kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa amejisikia vibaya kwa kilichotokea.

Mechi hiyo ilikamilika kwa ‘sekeseke’ kubwa ambapo kipa Antonin Kinsky aliokoa shuti la Sean Longstaff, huku Spurs ikinyimwa penalti baada ya James Maddison kuangushwa na Lukas Nmecha katika eneo la hatari.

Carragher anaamini kuwa pointi hiyo moja inaweza kuwa na faida kubwa kwa Spurs katika vita yao vya kubaki ligi kuu kwa msimu ujao.

SPU 03

Tottenham itashuka dimbani tena Jumanne ijayo kwenye uwanja wa ugenini dhidi ya Chelsea, huku wapinzani wao wa karibu West Ham wakitarajia kuchuana na Newcastle United katika uwanja wa St James' Park Jumapili hii.