Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CAF yatangaza faida nono

CAF Pict

Muktasari:

  • Ripoti hiyo inaonyesha mabadiliko makubwa ya kifedha kwa CAF, ambayo miaka mitano iliyopita ilikuwa inakabiliwa na changamoto kubwa za kifedha, ikiwa na madeni yaliyokuwa yamezidi Dola milioni 100.

ABUJA, NIGERIA: SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetangaza kupata faida ya jumla ya Dola za Marekani31.2 milioni (Sh80 bilioni) katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 2026, hatua inayoashiria kuimarika kwa hali yake ya kifedha chini ya uongozi wa rais wake, Dk. Patrice Motsepe.

Taarifa hiyo imewasilishwa kupitia ripoti ya hesabu za fedha ya mwaka 2026, iliyowasilishwa katika Mkutano Mkuu wa 48 wa CAF uliofanyika jijini Abuja, Nigeria, Jumamosi.

Ripoti hiyo inaonyesha mabadiliko makubwa ya kifedha kwa CAF, ambayo miaka mitano iliyopita ilikuwa inakabiliwa na changamoto kubwa za kifedha, ikiwa na madeni yaliyokuwa yamezidi Dola milioni 100.

Tangu alipochukua uongozi, Motsepe amesimamia utekelezaji wa mkakati wa kuimarisha hali ya kifedha ya shirikisho hilo, ukiwa na lengo la kuboresha usimamizi wa fedha, kuongeza vyanzo vya mapato na kuhakikisha CAF inakuwa na uwezo endelevu wa kujiendesha.

Matokeo ya mkakati huo yanaonekana kuzaa matunda, huku CAF ikiripoti kukusanya mapato ya jumla ya Dola milioni 284, sawa na ongezeko la zaidi ya asilimia 200.

Vilevile, akiba ya kifedha ya shirikisho hilo imeimarika kwa kiasi kikubwa, kutoka kwenye nakisi ya Dola milioni 16.8 hadi kuwa na salio chanya la Dola milioni 14.4.

CA 01

CAF imeeleza pia kuwa hadi mwishoni mwa Juni 2026 ilikuwa na fedha taslimu zilizofikia Dola milioni 118.8, hali inayoliweka katika nafasi nzuri zaidi ya kugharamia shughuli zake na programu mbalimbali za maendeleo ya soka barani Afrika.

Mafanikio hayo yanaonyesha mabadiliko makubwa ikilinganishwa na hali ngumu ya kifedha iliyokuwa ikilikabili shirikisho hilo miaka mitano iliyopita, huku yakitoa msingi imara zaidi wa kuendesha shughuli zake kwa uendelevu.

Mbali na kuongeza mapato na kurejea kwenye hali ya kupata faida, CAF imesema imeongeza kwa kiasi kikubwa msaada wa kifedha kwa wanachama wake 54, vyama vya soka vya kanda, klabu na mashindano mbalimbali.

Uwekezaji huo unatarajiwa kuchochea maendeleo ya soka barani Afrika kwa kutoa nguvu zaidi za kifedha kwa wadau wanaohusika na kukuza mchezo huo katika maeneo mbalimbali ya bara hili.

Takwimu hizo mpya zinakuja wakati CAF ikiendelea na juhudi za kuongeza thamani ya kibiashara ya soka la Afrika, kuimarisha mashindano yake na kutafuta mifumo endelevu zaidi ya ufadhili kwa vyama vya soka vya kitaifa.